Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,582
Pinda akiwepo mahala lazima hali ya hewa ichafuke tuu...
Jana kulikuwa na sherehe za kumuaga Samweli Sitta ,Spika za zamani wa Bunge zilivurigika baada ya Spika wa Bunge na Pinda kuamuru zipigwe nyimbo za Komba na mmojawapo uliopigwa ni ule wa ....wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe... Wimbo huu uliamsha hasira za wabunge wa CUF ambao waliamua kuondoka kwenye sherehe hizo bila kula chakula kilichokuwa kimeandaliwa.
Mbatia naye alitaka kuondoka ila akashikwa mkono na wabunge wa CCM naye bila aibu alirejea kwenye sherehe hizo , ila wabunge wa CUF waliamua kuondoka moja kwa moja pamoja na zawadi waliyokuwa wamemwandalia Sitta.
wabunge wa Chadema ,hawakuwepo hata mmoja .
Tatizo sio wimbo wa nani ila ni maudhui ya wimbo na hadhira kusudiwa, hivi unaendaje kuweka wimbo wa wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe , kwenye sherehe za kuaga spika aliyekuwa na wabunge wa upinzani na hao wa Ccm? Huu ni ujinga uliopindukia , sasa waliachiwa chakula chao walifurahia kula chote wenyewe?Hii nyimbo ingekuwa ni ya CUF au NCCR au TLP, DP, UDP ingekuwaje?
Wakati Pinda anakaribishwa alianza kwa kusema CCM hoyeee......mara kajishitukia akasema ila kwani hata nikisema hivyo kuna nini si ni salamu zetu? .........hiii ni dalili za wazi jinsi walivyo na chuki za ndani na watu ambao sio CCM .....Pinda ana akili finyu sana ukichanganya na ugonjwa anaoumwa basi ndo anakuwa kama msukule kabisaaa
Nadhani sasa ugonjwa unaadhiri mfumo wa fahamu..msameheni bure...
Kama waliberali walikasirika kiasi hicho sipati picha wangekuwepo CDM lazima kingewaka tu....CDM wangekuwepo wasingethubutu kupiga hizo nyimbo... Paka akiondoka, panya anatawala.
ukistaajabu ya pinda
utashangaa ya makinda
Hiyo ndo CCM ya wachovu wa mawazo aliyoyasema Nyerere kwenye kitabu chake cha "Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania"
Yaani Sitta naye anakubali kufanyiwa sherehe ya kuagwa? Je hizo nazo ni fedha za walipa kodi au michango yao binafsi? Wamesahau kwamba watoto wanakaa chini hakuna madawati na walimu wanawadai, na wagonjwa wanalala wanne wanne kwa kila kitanda? "ama kweli akili za kuambiwa changanya na zako!"