Sherehe za kidini mgeni rasmi kiongozi wa nchi isiyo na dini!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,903
2,884
wadau nahitaji kupata uelewa mpana juu ya jambo hili nimeskia kwamba mheshmiwa rais wa nchi amealikwa kua mgeni rasmi kwenye sikukuu ya idd elfitri ninachoelewa mimi nchi haina dini licha ya kua nchi haina dini rais wetu pia si muumini wa dini husika,sasa hao waliomwalika kama mgeni rasmi wana dhumuni gani? au ndio kwenda kuchomekea risala ya madai ya nchi kuongozwa kwa mfumo kristo?
 
Nchi haina dini lakini watu wake wana dini zao. Wengine hawana hizo dini za mapokeo.
Dini zote zinatambua mamlaka ya viongozi hata kama ni dini tofauti!
Leo wakristo wamekula sana pilau kwa ndugu zao waislamu!
 
mooods naomba juu Uzi uondolewe unaleta ubaguzi wa kidini mm ni mkristu tena rc lakini hilo halikubaliki ni ufinyu wakufikiri
 
wadau nahitaji kupata uelewa mpana juu ya jambo hili nimeskia kwamba mheshmiwa rais wa nchi amealikwa kua mgeni rasmi kwenye sikukuu ya idd elfitri ninachoelewa mimi nchi haina dini licha ya kua nchi haina dini rais wetu pia si muumini wa dini husika,sasa hao waliomwalika kama mgeni rasmi wana dhumuni gani? au ndio kwenda kuchomekea risala ya madai ya nchi kuongozwa kwa mfumo kristo?
Bado unafikra za ki ISIS sana kaka, serikali ya nchi haina dini ila wananchi wake wana dini ikiwa ni pamoja na viongozi wake acha hizo, huyo ni mkuu wa nchi anaalikwa na kila mwananchi na wa dini zote
 
Watawala wanahusika sana na amani ya waumini. maisha ya waumini wowote hutegemea sana utawala uliopo.
Kwa hiyo kukiwa na uhusiano mwema kati ya waumini na utawala nchi itakuwa mahali pazuri kuishi watu wote.
 
Hii ni ibada kwa wenye dini yao sasa mtu wa dini nyingine anashiriki ibada ya dini isiyokuwa yake
 
Nchi haina dini lakini watu wake wana dini zao. Wengine hawana hizo dini za mapokeo.
Dini zote zinatambua mamlaka ya viongozi hata kama ni dini tofauti!
Leo wakristo wamekula sana pilau kwa ndugu zao waislamu!
Kama Waislamu walivyokula Futari za ndugu zao wakristo.
 
Bado unafikra za ki ISIS sana kaka, serikali ya nchi haina dini ila wananchi wake wana dini ikiwa ni pamoja na viongozi wake acha hizo, huyo ni mkuu wa nchi anaalikwa na kila mwananchi na wa dini zote
Nadhani mtoa mada anaeleweka vibaya. Kiutaratibu BAKWATA humualika kiongozi wa nchi kisiasa katika barza la Idd. Wamefanya hivo tokea enzi za mzee ruksa ila sikumbuki kama enzi ya baba wa taifa mambo haya yalikuwepo.Mie kinachonistaajabisha ni kuwa waalikwa huwapa maagizo waalikaji ya kuhubiri AMANI ilhali waalikaji hawawapi waalikwa maagizo yoyote.
 
Speculations za namna hii ni hatar sana kwa afya ya akili hasa kwa nguvu kazi ya taifa hili. Tatizo la nchi yetu hata kuifanya kuwa masikini ni watu wake kuwekeza kujadili vitu vidogo sana visivyokuwa na impact yoyote katika maendeleo, watu ni wavivu sana na wanaishi kwa hisia, hao wanosema anapendelea sijui mfumo na wewe unayehisi hivyo mnatakiwa mpuuzwe kabisa. Kuna manufaa gani tukigawana vyeo kwa kubalance dini halafu utendaji ukawa hovyo? Hakuna muislam mwenye akili timamu, nimesema akili timamu'' anayewekeza kujadili usawa wa vyeo wakati ana jukumu la kufanya ibada kibao zisizokuwa na uhusiano wowote na vyeo.
 
Duuu! Mkuu yani ulikaa kabisa ukaanza kutapye na kutuma humu ndani watu tuanze kujadili na hili?.....your not serious aisee!
 
Back
Top Bottom