Sherehe ya Siku ya Kuzaliwa.

Sherehe ya Siku ya Kuzaliwa.

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Posts
18,830
Reaction score
12,312
Ivi kwanini watu huo wanahangaika kuandaa sherehe kuubwa ya kuziliwa afu hawasemi wametimiza miaka mingapi?

Hofu yao ipo wapi? kama unaogopa kuonekana kikongwe, kwanini ufanye sherehe?

Ivi kama mfano miaka yako ya kuishi uliopangiwa na Mnyaazi Mungu ni 70, je huoni umepunguza moja ya miaka yako hapa duniani?

Kama umepunguza miaka na siku zako za kuishi duniani,, unafanya lijisherehe la nini?

Je kama umezoea kufanya masherehe makubwa makubwa,, ukifa, wapendwa wako wataendelea kukumbuka siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya sherehe?
 
hizo siku za kuzaliwa hata mimi sijazifahamu hua wanasherehekea ajili gani?
Japo kila mtu anaweza kuweka mpango wake wakujifurahisha.
Wengina wasema wanakumbuka siku zao za kuzawa(kuzaliwa) kuja duniani.
Yaan hua nakosa majibu...
 
Yaani unakimbilia uzeeni afu unafurahia, hamjui fainali ni uzeeni?:second:
 
Hofu yao ipo wapi? kama unaogopa kuonekana kikongwe, kwanini ufanye sherehe?..

..na kuna wengine wanaogopa 'kuonekana' bado wadogo/watoto pia! Nadhani tunatofautiano juu ya nini ni masuala binafsi na kwa kiasi gani....japo kuna wengine wanaenda mbali sana!
 
Ivi kwanini watu huo wanahangaika kuandaa sherehe kuubwa ya kuziliwa afu hawasemi wametimiza miaka mingapi?

Hofu yao ipo wapi? kama unaogopa kuonekana kikongwe, kwanini ufanye sherehe?

Ivi kama mfano miaka yako ya kuishi uliopangiwa na Mnyaazi Mungu ni 70, je huoni umepunguza moja ya miaka yako hapa duniani?

Kama umepunguza miaka na siku zako za kuishi duniani,, unafanya lijisherehe la nini?

Je kama umezoea kufanya masherehe makubwa makubwa,, ukifa, wapendwa wako wataendelea kukumbuka siku yako ya kuzaliwa kwa kufanya sherehe?
bora hata we bro jambazi husherehekei.. kwani ungekuwa unapunguza miaka kumi kabisa..THTHT
 
nadhani zinawafaa zaidi watoto ambao hujiona wamekuwa wakubwa zaidi...watu wazima ni zoezi la public relations tu ili kuleta watu pamoja for a reason. lakini kimsingi hakuna haja ya kusheherekea kitu kama hiki...
 
wazee ukisema ni lini mwisho wa mwezi ufike upate mshahara ndio hivyo unasema ni lini siku yangu ya kufa inakuja
 
Back
Top Bottom