MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 10,137
- 15,091
Wameshakuona wewe bwe*e....
Pole sana mapema hii wameshaanza kukuendesha
Pole sana mapema hii wameshaanza kukuendesha
Nilishawahi kuagizwa hii kitu na jirani yangu. Natoka zangu mjini mara napigiwa simu. Kaniagiza vitu vingi kidogo ila hila hichi akawa anasita kusema. Mimi nikadhani kusita kunasababishwa na gharama ya hicho kitu!! Mimi nikamwambia aseme, akasema tena akasema nunua ndogo sio kubwa. Mimi nikajitoa ufahamu na kumnunulia. Nafika tu na kumkabidhi mzigo, naona anakenua meno tu. Mimi nikajifanya kama naona kawaida
Mwe!
Huko mnakoishi na jirani yako hakuna maduka mpaka apigiwe anayetoka mjini aje na pad?
Tabia ya huyu dada wa mchumba wangu kunipelekesha kama gari bovu itasababisha mapenzi na ndugu yake yafe kwani imeshakuwa kero.
Anavyopiga simu utadhani yeye ndo mchumba wangu.
Mara utasikia niletee chips mara uko wapi na wafanya nini? mara hebu njoo hapa nyumbani mara moja na usipoenda kosa utasikia waringa sana au wewe wajishaua nini.
Leo nilikuwa naongea na ndugu yake akajua nimekata simu akaanza kuropoka anamwambia ndugu yake tatizo wewe wamchekea sana uyo X wako kwana mwambie mimi nina hamu na chips na soda.
Kwa tabia hii kama nikimuoa ndugu yake si atanipelekesha mpaka basi.kwa kweli mdogo wake hana tatizo lolote tatizo lipo kwa huyu ndugu yake.
nimechoka.
ushauri please.
Nilishamhisi kitambo anataka kitu, sema siku ile alinipa uhakika wa nilichokuwa nawaza