Shemeji kakubali nifanye nitakalo

Shemeji kakubali nifanye nitakalo

wakyagara wakinyora

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Posts
735
Reaction score
288
Wadau natumain hamjambo,

Nina rafiki yangu ambaye ni kama ndugu,tumetoka mbali sana na sasa ni kama mtu na kaka yake.jamaa yangu huyu(hajaoa) alikuwa na dem mmoja hivi lakini walishindwana kwa matatizo yao binafsi wakawa wameachana kama mwaka mmoja uliopita.

Kwa kuwa nilikuwa nishatambulishwa kwa shemej yangu huyo basi hata baada ya kuachana na jamaa yangu tukawa tunasalimiana,iko siku ananipigia na mimi kuna siku nampigia kumsalim. Tunaitana shemej.

Kuna kipindi shemej yangu huyo alikuwa na shida ya vijisent,kwa kuwa hakuweza kumwambia ex wake basi aliniambia mimi lakini nilimtonya ex kuwa mwenzake alikuwa na shida,jamaa hakutaka kumsaidia kabisa ex wake,nikachukua jukumu la kumsaidia huyo shem wangu.basi mawasiliano yakawa yapo kama kawaida kwa shem wangu huyo. Kuna siku shem aliniuliza kama wyf yupo home,nikamwambia alikuwepo lakini keshaondoka kurudi kazini kwake mkoa ana kama miez miwili sasa.

Basi shem akawa akinipigia simu hadi nyt kali kunisalimia na kunitakia usiku mwema. Mwisho wa siku shem akaniuliza nawezaje kuishi muda wote huo wakati wyf hayupo? Nikamjibu navumilia tu, akaniambia kweli huo ni muda mrefu ila endapo nitakuwa na shida yoyote yuko tayar kunisaidia,nanukuu;"nakuonea huruma shem wangu, muda huo ni mwingi sana kwa mwanaume,endapo utahitaji kampani yangu niko tayar kukusaidia kwa lolote wakati wyf hayupo,kwani hata huyo jamaa yako mi siko nae tena,hata mimi nilishapata mtu mwingine japokuwa kwa sasa hayupo,atarudi januari mwakani".

Niliingiwa na uoga sana lakini nikajikaza na kumwambia jamaa yangu kuwa ex wake kanipa ofa ya kapani yake na niitumie nitakavyo, jamaa akanijibu kuwa yeye alishamalizana nae, na hana sababu tena ya kurudiana nae, kama nina uwezo wa kutumia ofa hiyo basi niendelee nayo.

wadau hiyo ndo situation niliyonayo kwa sasa,naomba mwenye ushauri mzuri zaid na wa manufaa anisaidie
 
Na hili unahitaji ushauri bro? Ulilaimishwa kuoa?

Jaribu pia kuwaza wife naye anampa ofa mwanaume mwingine wa miraba minne...

NB: Jambo usilotaka kufanyiwa usiwafanyie wengine. (Do unto others what you would have them do unto you)
 
Mwanawake akitaka jambo! Ngumu kwa vijana wa siku hizi kuchomoka.
 
Sikushauri kufanya uasherati, hayo madude achana nayo...kila unapopenda mwanamke asie mke wako ni kukaribisha tatizo, huyo ni malaya...acha tu, kama unazidiwa panda gari nenda kwa mkeo ukatulize ngenye zako huko
 
Mkeo naye, jana tu kanipigia simu ananiomba ushauri kuwa wewe upo naye mbali kwa muda mrefu ujao sasa ameniomba nimsaidie kumtoa upweke. Je nikubari au nimpotezee?Jibu lako litakupa go ahead kumgegeda huyo shemeji yako kwa maana hata kama ukijakutufuma itakua hamna sababu ya kutu laumu maana zinaa hulipwa kwa zinaa.
 
Achana nae kaka ukianza kutoka nae tu atakubana hadi mkeo ajue hana wema huyo piga chini kabisa
 
Achana na huyo demu atakufanya ukosane milele na huyo jamaa yako ambaye ni wa muhimu kuliko huyo demu.

Demu anachotaka hapo ni msaada wako na jiulize kwa nini aliachana mshikaji.
 
Habari uliyoandika iko tofauti na kichwa cha habari yenyewe. "Shemeji kakubali nifanye nitakalo" ina maana wewe ndio uliyemuomba kufanya utakalo, kwahiyo wewe ndio uliyeanza kumchokoza. na mkeo huko aliko akisoma hii habari itakuwaje? au hakuna mtandao?

Naona kama unatuletea hadithi zisizo na mantiki hapa.
 
Umeshajadiliana na mkeo kabla hujataka ushauri wetu? Kama tayari tunaomba utuwekee ushauri wake kisha tuongezee ila kama bado tafuta kwanza ushauri kwa mkeo kwa kuwa ndio utakaoamua mustakhabali wenu!
 
kamuombe ushauri diva loveness love ....huku tuna mambo mengi ya kufanya
 
Back
Top Bottom