Shemeji ananitaka

Shemeji ananitaka

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,363
Reaction score
16,092
Habari za muda mrefu wana jukwaa. Iko hivi nina rafiki yangu yeye ana mtoto mmoja yaani single mum, sasa ana mwanaume wake. Huyo mwanaume wake kipindi wanaanza mahusiano hata mimi nilikuwa nawaona mpaka sasa wamefikia kama miaka kadhaa ya mahusiano yao.

Huyu mwanaume siyo baba wa mtoto wake, sasa huyu shemeji kuna siku moja alichukua namba yangu nikiwa pale kwa rafiki yangu, yeye rafiki yangu alikuwa jikoni anapika, mimi nilijua kachukua kwa nia nzuri tu awe anakuja ofisini labda kuniungisha.

Sasa tulikuwa tunawasiliana akawa ananiita mke mdogo, mara ananiambia nimzalie mimi namwambia siwezi kufanya hivyo wewe ni shemeji yangu nakuheshimu, anasema kwani kuna ubaya. Mara kuna kipindi anakuja ofisini ananiambia wameachana na rafiki yangu mara warudiane.

Huyu shemeji nimemuona ni mtu wa ajabu sana kwa kitendo cha kunitaka kimapenzi kwani huko kote hajaona wanawake hadi aje kwangu, kwa rafiki wa mtu wake, wanaume hamna haya kabisa.

Mimi sijawahi kumwambia rafiki yangu na nimekata mazoea nao wote wawili, maana rafiki yangu akijua tu nilikuwa nachat na mtu wake atakasirika mno maana ana wivu balaa.
Cc. holoholo
Nomadix
 
Nikawaida sana kwetu sisi wanaume, na tunatabia ya kujaribi pale tubapo ona tako ama titi limechangamka..😋
Misioni kesi hapo, wekausha mkuu wala usiwaze
Ila nyie wanaume kwanini hamna adabu sasa jamani, rafiki yangu ni kamodo flani hivi anampikiaga misosi mitamu anaenjoy tamaa za nini tena huku nje
 
Back
Top Bottom