Mkuu pole sana na hilo lililokupata, chamsingi hapo kama suala linaukweli wowote, tumia hekima ya hali yajuu. Mosi, mkeo kashindwa kuilinda heshima yako; Pili mkeo kavunja uaminifu kwakutembea na shemeji yako hiyo nidharau kubwa sana pia nakupongeza kwa uvumilivu, ingekuwa mimi tungekuwa tunaongea mengine sasahivi. Tatu nadhani mkeo hana malezi ya kutosha toka kwao ndomaana anadiriki kukuvunjia heshima kiasi hicho. Nini kifanyike? Ili kuepuka fedheha na kama haya unayo yaongea yanaukweli wowote, huyo mwanamke safiri nae mpaka kwao mkiwa na zawadi kedekede kwaajili ya wazazi, mkifika kule lala sikumoja kesho yake asubuhi kabla hawajatawanyika kwenda kwenyemihangaiko, waambie unataka kuwaona kwa dakika tano, wakiridhia waambie nia na madhumuni ya kuja nikwaajili ya kuwakabidhi binti yao asiye na adabu, taja vyote ambavyo amekufanyia. Baada ya hapo rudi kwako na kisha uende angaza kucheki afya kama itakuwa fiti. Kama upo safi subiri, Mwenzi wako anakuja na yule ulibugi tu. Kila la heri!!