Shellukindo matatani Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shellukindo matatani Dar

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Feb 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]
  Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo​
  Elias Msuya na Leone Bahati
  MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ametakiwa kuripoti katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ifikapo Machi 7 mwaka huu, ili kusikiliza hukumu ya kesi ya madai inayomkabili.

  Shelukindo anadaiwa kushindwa kulipa mkopo aliouchukua kutoka kwenye benki ya Azania mwaka 2005.
  Hakimu wa mahakama hiyo, Joyce Minde alisema hukumu ilishatolewa na mahakama hiyo ambayo ilimamuru Shellukindo kulipa deni analodaiwa na benki hiyo, lakini hadi sasa ameshindwa kutekeleza amri hiyo.

  “Hiyo kesi siyo ngeni, ni kesi ya madai namba 92 ya mwaka 2005 na ilishatolewa hukumu. Tunachofanya sasa ni kukazia hukumu tu,” alisema Minde na kuongeza:

  “Kuna njia mbalimbali za kukaza hukumu kama vile kukamata mali za mdaiwa, mfano nyumba au kufungwa jela.”
  Alisema; “Nitasikiliza utetezi wake na nitatoa hukumu kulingana na uzito wake. Kama hauna uzito mahakama itachukua hatua kali, ili alipe deni hilo.”
  Hata hivyo, Minde hakuweka wazi kuwa hukumu ya kwanza ilisomwa lini kwa maelezo kuwa, yeye hakuwapo wakati hukumu hiyo ilipotolewa.

  Kwa upande wa Benki ya Azania inayomdai Shellukindo, haikuwa tayari kueleza kiasi cha fedha inachomdai wala mwenendo wa kesi hiyo huku wasemaji wa benki hiyo wakielezwa kuwa kwenye vikao kwa muda mrefu.

  “Ni kweli hiyo kesi ipo, lakini mimi siyo msemaji. Kwa sasa wasemaji wa benki wako kwenye kikao cha muda mrefu, labda ufuatilie huko huko mahakamani ” alisema mmoja wa watumishi wa benki hiyo anayefanya kazi katika kitengo cha sheria ambaye hakutaka kutaja jina lake.

  Shellukindo ajibu
  Alipotakiwa kuzungumzia kesi yake hiyo, Shellukindo alisema hana taarifa kwamba mahakama imemtaka afike mahakamani hapo Machi 7 kusikiliza kesi hiyo.

  "Mimi sina taarifa yoyote kwamba natafutwa," alisema Shellukindo akielezea kushangazwa na jinsi jambo hilo linavyopewa umuhimu mkubwa na vyombo vya habari kwa kile alichosema, "We ni mwandishi wa kumi unanipigia kuniulizia juu ya jambo hilo."

  Alikiri kuwa ni kweli ana deni analodaiwa na benki hiyo na kwamba, suala hilo siyo la ajabu kwa sababu ni Watanzania wengi wamekopa benki na wanadaiwa hivyo anashangaa kuona yeye kukopa imekuwa ajabu.

  Hata hivyo, alitafsiri suala hilo kuwa ni mchezo unaochezwa na maadui zake kisiasa kwa lengo la kumchafua na kushusha heshima yake mbele ya jamii.

  Shellukindo alienda mbali akiwatuhumu baadhi ya waandishi wa habari wanaolifuatilia suala hilo kwamba wamehongwa ili kumchafua."Siyo ajabu sasa watakuja wachunguze mimi na mume wangu tuna ndoa au la," alilalamika Shellukindo.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo.Shellukindo matatani Dar
   
 2. B

  Bandio Senior Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hah! Hata wahishimiwa nao wako hivyo? Kumbe ndio maana huduma za mikopo zinazotolewa zinakuwa na masharti magumu kwa sababu ya watu kama hawa. Asante mkuu nimejifunza kitu hapa.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Alikwenda kwa nabii Joshua kule Nigeria kuombewa deni lake lifutwe!! Angekuwa na akili angetumia zile fedha za nauli kupunguza deni lakini kwa vile hamnazo ndio hivyo!!
   
 4. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watanzania hawaaminiki katika mikopo.. Ndio maana taasisi za fedha zinatoa masharti magumu na kutoza riba kubwa kufidia wakimbiaji
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Hapa ninachoona ni kwamba hawa "wakubwa" wengi sana wana ma-issue kama haya, ila Tanzania hakuna ufuatiliaji hususan ukiwa mkubwa.

  Sasa ukiwa unajifanya unaanzisha chokochoko, unajua kuwasema na kuwachimba wakubwa wa CCM, watu wanavuta faili lako na kuangalia waanze wapi kukuumbua. Hiki ndicho kilichotokea hapa. Wewe huwezi kujiuliza miaka yote hiyo walikuwa wapi mpaka leo huyu mama anasemekana kuleta chokochoko ndani ya CCM ndiyo wanafukua madai?

  Hivi huyu mama angekaa kimya na kuheshimu uongozi wa CCM tungesikia haya?

  Nilikuwa na mshua mmoja wa N.I.C, tukawa tunapiga stories za kazi etc. Akanipa story jinsi N.I.C "ilivyoikopesha" CCM hela kibao, enzi za "chama kushika hatamu", basi huyu mzee akawa anamkumbushia Rashid Mfaume Kawawa kuhusu lile deni, Kawawa akamjibu "kwani nyinyi hamna "bad loans" huko N.I.C? Akaambiwa bad loans zipo kila mahali. Kawawa akamjibu basi weka mkopo huo katika "bad loans".

  Yaani kuna wabunge na wakubwa wa chama na serikali kibao walishajua "mkopo" ni jina lingine la posho tu, hawana mpango wa kulipa.

  Sasa wakijisahau na kuanza kupaka, watu wanafukua mikopo mpaka ya 1980's huko na mikopo ya benki ya nyumba iliyowapatia kina Nyerere nyumba ya Msasani na kina Mkapa nyumba ya Upanga nyuma ya Olimpio pale.

  Ambayo mingi haijalipwa.

  Nyerere mwenyewe hajalipa mkopo wa benki ya nyumba uliompa nyumba ya Msasani, na huyu ndio mtu tunaemuona principled. Kisingizio eti walimkatalia kulipa.

  Mimi ningetaka kuona uchunguzi unaanzishwa kuangalia wafanyakazi wote wa serikali na vyama vya siasa waliochukua mikopo nahaijalipwa. Siyo kumfuatilia mtu kwa sababu kawapaka au anataka kumtoa Kikwete uenyekiti CCM tu.
   
 6. B

  Bandio Senior Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa napo kuna kitu cha kujifunza, thanks mkuu.
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wabunge nao wanashindwa kulipa mikopo na mihela yote ya posho wanapeleka wapi
  sisi wa kima cha chini si ndio kwisnhey kabisa
   
Loading...