kwa mujibu wa vyanzo mbalmbali vya habari:
=aliwahi kutabiri vita dhidi ya nduli iddi amini, ikatokea
=aliwahi kutabiri moto kuwaka juu ya maji ikatokea kule goma drc
=aliwahi kutabiri mwanamuziki mwenye upara kufariki ghafla akiwa ******, utabiri huo ukamuangukia brenda fasi wa kule afrika ya kusini
=aliwahi kutabiri mwanmuziki maarufu kutoka nchi jirani aliyefungwa kuachiwa huru, wengi walidhani angekuwa ni babu seya, lakini utabiri huo ukamuangukia papa wemba wa kule drc aliyefungwa kule nchini ufaransa kutokana na kuingiza wahamiaji haramu kupitia bendi yake.
=aliwahi kutabiri rais wa awamu ya tatu mheshimiwa benjamini mkapa kuongezewa muda wa kuongoza nchi hata bada ya muda wake kuisha, wengi wakapiga kelele, lakini mwishowe ikatokea bada ya kifo cha mgombea mwenza wa chama kama sikosei tlp au chadema na uchaguzi ukasogezwa na hivyo rais wa wakati huo mheshimiwa mkapa akajikuta akiendelea kuongoza kwa muda zaidi ya kipindi chake, utabiri huo ulitimia.
=alitabiri kifo cha makamu wa rais hayati dr. Omari ali juma na utabiri huo ulitimia.
kwa kifupi zipo tabiri nyingi ambazo zilithibitishwa kutokea na hizi ni miongoni mwa tabiri hizo.
kwa kifupi utabiri ni utaratibu wa kudadavua kitu ambacho aidha kinaweza kutokea au kisitokee kulinga na mazingira.
taaluma hiyo ni ya kujifunza na mtu yeyote anaweza kujifunza akipenda.
lakini hata hivyo umri nao unaweza kuchangia kiwango cha ufanisi kupungua na ndio sababu ya sheikh yahya kupoteza umaarufu, na ndio maana hata serikali kuweka umri wa waajiri wetu kustaafu, kutokana na kuchoka kiakili na kimwili. Hata hivyo hilo limeshindikana kutokana na watu wengi waliostaafu kutoka serikalini kukimbilia kwenye siasa. Inashangaza kidogo kwa kuwa kama mtu ameshindwa kwenye utumishi wa umma atawezaje uleta tija kwenye siasa.
naona sasa ninachanganya mada, ngoja niishie hapa.