Sheikh Yahya awatabiria mabaya wanasiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Yahya awatabiria mabaya wanasiasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Apr 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  na Hellen Ngoromera


  MNAJIMU Mkuu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amewatabiria viongozi wa siasa na wafanyabiashara maarufu kutekwa nyara.
  Sheikh Yahaya amewatabiria pia viongozi hao, wake zao au maswahiba zao kuibiwa na kufanywa kama bidhaa.
  Alisema hayo jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kuhusu utabiri wake wa mwezi huu.
  “Kuanzia Aprili 19 na kuendelea hadi Julai, viongozi wa siasa na wafanyabiashara maarufu wajichunge kutekwa nyara na kuibiwa, wao wenyewe na kufanywa kama bidhaa.
  Aliwataka wachukue tahadhari hasa wanapotembea na kusafiri kwani kuna uwezekano wasirudi mara watakaposafiri.
  Utekaji nyara huo ni wa viongozi tuliowataja na wasijiamini wanaposafiri au wakiwa kwenye mikutano wasiwe peke yao na wawe na mipangilio ya tahadhari nyakati zote. Kwa mujibu wa Sheikh Yahaya ambaye amekuwa akitabiri mambo mbalimbali, nyota hizo pia zinawalenga wake na maswahiba wa viongozi hao mashuhuri.
   
 2. a

  allydou JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,485
  Likes Received: 572
  Trophy Points: 280
  kwani huyu si alishaacha utabiri, au inakuwaje waseee.
   
 3. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Mbona hakuna mgombea urais aliyekufa kabla ya uchaguzi 2010? Asituzingue!
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mpango ule ule wa kuwatisha watu wasifanye siasa. Amefanya jambo la maana sana kufahamisha wazalendo kuwa kuna mpango wa kuteka nyara viongozi wanaoipinga serikali. Wakifika huko basi wajiandae maana ni lazima ita-backfire tu.
   
 5. Bassanda

  Bassanda Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 6. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo kwenye red hapo!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  yale yale ya gazeti la mwanahalisi huyu jamaa itabidi atiwe ndani afu tuone utabiri wake utuaje...
   
Loading...