Sheikh Yahya awashukuru vigogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Yahya awashukuru vigogo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 25, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  MNAJIMU mashuhuri nchini, Sheikh Yahya Hussein, amewashukuru marais wastaafu wa Awamu ya Pili na ya Tatu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, kwa kumsaidia wakati alipokuwa mgonjwa kisha kupelekwa nje ya nchi kutibiwa.

  Sheikh Yahya alitoa shukrani hizo juzi usiku alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Nyota Zenu kinachorushwa hewani na kituo cha televisheni cha Channel Ten.

  Kwa mujibu wa mnajimu huyo, anamshukuru Rais Mkapa kwa kumsaidia wakati Rais Mwinyi anamshukuru kwa kumpigia simu na kumjulia hali pamoja na Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban bin Simba.

  “Namshukuru pia ndugu Mengi (Reginald - Mkurugenzi wa makampuni ya IPP), yeye pia alikuwa akinijulia hali, lakini alinilaumu kwa kuondoka bila kuniaga,” alisema Sheikh Yahya.

  Sheikh Yahya ambaye amejizolea umaarufu ndani na nje ya nchi kutokana na kazi yake ya utabiri, alimshauri Mufti Sheikh Mkuu kudai kwa nguvu suala la Mahakama ya Kadhi.

  Alitoa changamoto kwa Waislamu wote nchini kutotumia misikiti kudai Mahakama ya Kadhi bali watumie vyama vyao kudai suala hilo.

  Leo Sheikh Yahya anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari masuala mbalimbali kuhusu kazi yake ya utabiri.
   
Loading...