Sheikh wa mkoa wa Dar (Bakwata) amshukia Mbunge

Sheikh wa mkoa wa Dar (Bakwata) amshukia Mbunge

5523

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2014
Posts
2,290
Reaction score
2,431
Mbunge wa Konde Khatib Said Haji (CUF) amemtaka Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, kujitafakari na kujipima kama chombo anachokiongoza cha Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kipo kwa ajili ya kuwalinda na kuwasaidia waumini wa dini hiyo au kimegeuka chombo cha kuwatetea wanasiasa hususani wa CCM na serikali yake.

Hivi karibuni Sheikh Salum alikaririwa na gazeti mmoja (siyo NIPASHE), akiwataka Waislamu nchini kumpuuza Mbunge huyo kwani ni mfitinishaji kwa Waislamu.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge, Haji alisema licha ya Bakwata kuwa ni chombo cha kutetea maslahi ya Waislamu na kuwaweka katika masuala ya kiroho lakini kutokana na uongozi mbovu kwa sasa chombo hicho kimegeuka kuwa ni mtetezi wa viongozi wa kisiasa na kuwakingia kifua viongozi wa serikali.

Alisema amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia Sheikh Salum kumwita mbunge huyo mfitini kutokana na kutokubaliana na utendaji wa chombo hicho ambacho kwa sasa kinaonyesha kukiuka maadili ya Bakwata na kujiingiza katika siasa.

"Bungeni niliwahi kusema kuwa Bakwata ni taasisi ya kinafiki kwa waislamu…kauli yangu hii itabaki kuwa pale pale na wala sitoibadilisha," alisema na kuongeza:

"Nasema kuwa viongozi wengi wa Bakwata kazi yao kubwa ni kusubiri kupokea kondoo kutoka Uarabuni kwa ajili ya kuchinja huku wakijinufaisha wao viongozi badala ya kuangalia ni jinsi gani ya kuwasaidia waumini wa dini ya Kiislamu."

Alisema waumini wa dini hiyo wanatakiwa kumpuuza Sheikh huyo kutokana na kauli zake ambazo anazitoa juu yake (Haji).

Chanzo:Nipashe
 
Huyu shehe na yule mwenzake mattaka hawa ni mashehena, pamoja na bakwata yote,

Bakwata imeasisiwa na ccm hapo wanatekeleza ilani
 
Sheikh wa mkoa yuko Dar pekee?! Yeye ahami, habadirishwi au naye cheo chake ni mpaka afe kama yule sheikh mkuu wa bakwata?!
Huyu alichaguliwa au aliteuliwa?!
Wa wilaya nani?!
 
Mbona mnafukua makaburi ya mbali hvyo
 
Sheikh wa mkoa yuko Dar pekee?! Yeye ahami, habadirishwi au naye cheo chake ni mpaka afe kama yule sheikh mkuu wa bakwata?!
Huyu alichaguliwa au aliteuliwa?!
Wa wilaya nani?!
Wanateuana tu kwa vigezo wanavyovijua wenyewe bila hata ridhaa ya waislamu
 
Sheikh wa mkoa yuko Dar pekee?! Yeye ahami, habadirishwi au naye cheo chake ni mpaka afe kama yule sheikh mkuu wa bakwata?!
Huyu alichaguliwa au aliteuliwa?!
Wa wilaya nani?!
Yaani miaka yote sheikh wa mkoa ni yeye tu, Sijui hakuna wengine wenye elimu ya dini,, Huu ndio udikteta wenyewe sasa
 
AKIJICHANGAYA TU SIKU KUSWALISHA AJUE KANIPA KESI COZ LAZIMA NIMTOE HALAFU NIMPASUE.TULIOSOMA KINONDONI MUSLIM SHULE YA BAKWATA O LEVEL TUNAMJUA TENA UCHAFU WAKE WA SASA HIVI UNA AFADHALI MAANA ZAMANI ALIKUA ANALIWA NA WENGINE WALIKUA WAKIMUONA ANASWALISHA WALIKUA WANATOKA WANASWALI PEKE YAO
 
Yaani miaka yote sheikh wa mkoa ni yeye tu, Sijui hakuna wengine wenye elimu ya dini,, Huu ndio udikteta wenyewe sasa
Kwani wana katiba kama NGO au wao wanafuata ILANI kama wenzao?!
Sijui anaswalisha msikiti gani?!
 
Back
Top Bottom