Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 980
- 3,646
Sheikh Ponda akizungumza na wananchi mkoa wa Temeke katika mkutano wa ACT Wazalendo amesema kuwa
Viongozi wa dini kushiriki siasa linatafsiriwa kama jambo geni kwa sasa, lakini kiuhalisia siyo geni. Katika Historia ya nchi yetu, chama cha kupigania uhuru kimeanza 1929 cha Africa Association, waasisi wa AA miongoni mwao ni viongozi wa dini akiwepo Mufti Hassan Bin Amir hii ni kwa upande wa Tanganyika.
Lakini kwa upande wa Zanzibar chama kilicholeta uhuru ni Zanzibar Nationalist Party, kiongozi mkuu wa chama hicho alikuwa Sheikh Ali Muhsin Baruani.
Kwa muhtasari, viongozi wa dini ndio wabunifu wa fikra za kupigania uhuru. Na wameshiriki katika harakati za uhuru na kujenga nchi kwa miaka mingi.
Hapa Tanzania, viongozi wa dini wameondolewa katika siasa mwaka 1963, baada ya kuwaondoa, ndio wakaanzisha hiyo propaganda kwamba dini na siasa ni vitu tofauti havifungamani na kwamba viongozi wa dini hawarusiwi kushiriki siasa.
Hii ilikuwa ni dhulma ya makusudi ambayo ilifanywa na wanasiasa kuwatoa waaasisi wa harakati za siasa viongozi wa dini katika siasa.
Historia inaonesha viongozi wa dini wanashiriki siasa, na hawa niliowataja siyo viongozi wa dini wa kawaida, ni maulamaa.
Mimi ninashiriki kwasabau nina ushahidi kutoka kwa hao viongozi waliotangulia, na sitoacha kushiriki siasa. Kuna lugha imetumika hapa, hatuwezi kumwachia fisi bucha, na sisi viongozi wa dini hatuwezi waachia fisi bucha kwa maana ya wale viongozi ambao hawataki tushiriki siasa.