Mzee Msemakweli
Senior Member
- Oct 12, 2010
- 159
- 34
Mimi sioni tatizo kujua idadi ya dini na waumini wake hapa nchini mbona nchi zingine takwimu kama hizi zipo wazi kuna nini Tanzania?
wanataka idadi yao ili takwimu hizo hizo wazitumie kuwauwa wakristo. kwasababu sensa si itaonesha wakristo ni akina nani? mt ni mtz ya nini kujua dini yake inasaidiaje maendeleo ya nchi? hebu mashehe mtuambie mna malengo gani ya kujua waislamu wako wangapi?Nenda ukaishi kwenye hizo Nchi zinazowahesabu watu wake kwa DINI zao. Tuondelee ujinga wa kila mara kutaka kuiga mambo yanayofanywa na Nchi zingine. Mbona Nchini Syria Majeshi ya Serikali yanawatwanga Wananchi wake. Je na sisi tuige hilo? Nchi za Magharibi zinaruhusu ndoa za jinsia moja, je na sisi turuhusu hilo? Acha kuangalia wengine wanafanyaje kwao angalia wewe unataka kufanya nini.
Mfano wako wa Israel na Palestina sio sahihi, Israeli wangeachwa peke yao wangeshatandikwa siku nyingi na Wapiganaji wa Kipalestina, ila kwa vile Israel inasimamishwa na mataifa ya Magharibi, USA, UK nk
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu (Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali kuhesabiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba, inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.
Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wengi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.
"Waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa," alisema Shekh Ponda.
Hivi karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Chanzo: Nipashe
Huyu Sheikh amezipata wapi hizo takwimu kwamba 80% ya Waislamu TZ ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote? Halafu baada ya Sensa ya dini ikajulikana waumini wa dini fulani ndio majority italisaidiaje Taifa? Ninaamini kuwa wapo waislamu wengi Tanzania wasioyumbishwa na kauli na misimamo ya viongozi wao, lakini viongozi wa aina hii wana mchango gani kwenye ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla?
kazitoa kwenye kijiwe cha kahawa.....
Izo Zama za Kutangaza Dini kwa kutumia Energy (nguvu) zishapitwa na wakati..hasitake kuwafanya waislam wote wajinga..Kama kweli Mshika Dini kwa asiendelee Mawaidha yenye kujenga Dini..
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mfano wako wa Israel na Palestina sio sahihi, Israeli wangeachwa peke yao wangeshatandikwa siku nyingi na Wapiganaji wa Kipalestina, ila kwa vile Israel inasimamishwa na mataifa ya Magharibi, USA, UK nk
Hivi idadi kubwa ya waumini wa dini bila kuwa na uwezo kiakili inasaidia nini katika Dunia hii? Hivi idadi kubwa ya wapalestina imesaidiaje kuwaondoa katika makucha kandamizi na utwala wa waisraeli? Hivi bado hatuwaoni wamasai na wasukuma mtu mmoja avyoswaga kundi la makumi ya ng'ombe?
Ndugu zangu tuache ujinga wakujitambulisha na kutengana kwa kufuata dini za wakandamizaji na wanyanyasaji. Kila siku najiuliza itakuaje babu zetu wale walio hasiwa kwenye bandari za bara Arab wakiamka na kuwakuta wakina sheikh Ponda na misimamo Yao ya KUWATENGA ndugu zao waafrika weusi na kuwakumbatia waarabu na dini yao?
are u sure kwamba israeli inasapotiwa na west country je?palestina haina marafki fuatlia ujue who are jews,ukjua ndo utoe comment.:A S-baby:
mi napendekeza waweke huo udini wao, ili tufuatilie nyendo zao. nimechoka na kelele zao. kuna mmoja alitoa ufafanuzi kuwa, eneo la kiseke mwanza, maeneo ya huduma za jamii, wakati wakristo wametengewa zaidi ya hekata 1,000 kufanya shughuli za kijamii kujenga makanisa na mambo memngine yanayowahusu, waislamu wametengewa hekata 100 tu. sina hakika na takwimu hizi, lakini akasisitiza, kilichosababisha utofauti wa ukubwa wa maeneo, ni kwa kuwa serikali ina takwimu za idadi ya watu kwa kuzingatia dini zao kitu ambacho hakijawahi kufanyiwa kazi tanzania.
mimi nilimjibu nikamweleza kuwa, waislamu kuna madhehebu makubwa manne, wakati wakristo utahesabu madhehebu hadi utachoka. kiukweli sijui idadi ya madhehebu kwani yaliyopo si chini ya 50 kwa yale ninayoyafahamu. kwa hiyo iwapo kila dhehebu litaomba kiwanja huko kiseke, hata hizo hekata 1,000/ hazitatosha, lakini waislam kwa idadi ya madhehebu yao, wana uhakika wa kupata kila dhehebu hekta 25, ambalo ni eneo kubwa mno.
sasa kama wanahisi wananyanyaswa katika kugawa rasilimali za taifa, tuhesabiwe kwa dini zetu ili tuone mwishoni itakuwaje
HAYA NI MAKADILIO YA KIMATAIFA KWA WATU WALIOSOMA RESEARCH WATANIELEWA. Si lazima Kumfuata Mtu na Kumuuliza..
WE TAKE SAMPLE
Sensa ya 1967
Takwimu ya dini nchini Tanzania kwa sasa haipatikani kwa sababu maswali kuhusu dini yaliondolewa na serikali katika sensa baada ya
mwaka 1967. Sensa ile ya tarehe 27 Agosti ilihesabu wafuasi wa dini za jadi kuwa 34.3%, Wakristo 33.5% na Waislamu 31.4%, mbali na wengineo 0.8%.[1]
BAADA YA HAPO
"World Christian Encyclopedia" (toleo la pili, Oxford 2001) imekadiria kwa mwaka 2000 Wakristo kuwa 50.4 % (Wakatoliki 24.7%, Waprotestanti mbalimbali 16.5%, Waanglikana 7.9%, wasio na madhehebu maalumu 3.5%, madhehebu huru 1.9%, madhehebu yasiyokubali imani ya msingi ya Wakristo wengine wote 0.1%, wenye kufuata madhehebu mawili kwa wakati mmoja 4.2%),
Waislamu 31.8%, wafuasi wa dini za jadi 16.1% na wengineo 1.8%.
Pia imetabiria kwa mwaka 2025 uwiano kuwa 56.1, 32.8, 8.9 na 2.1%, na kwamba kufikia mwaka 2050 Wakristo na Waislamu watakuwa karibu 65 na 35% kati ya wakazi wa nchi.
Taarifa ya "International Religious Freedom Report 2009" kutoka Marekani Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor
kwa mwaka 2009 unaotaja 62% ya Watanzania kuwa Wakristo, 35% Waislamu na 3% wafuasi wa dini nyingine.[4]
mkuu israel ni taifa teule la mungu na hakuna awaye yeyote wa kulishinda taifa hili kwani mungu alisema taifa lelote litakarolibariki taifa la israel basi nalo litabarikiwa na taifa lolote litakaloilaani israel basi nalo litalaaniwa ndio maana wenzetu wa mataifa ya magharibi walishalitambua hilo mapema ndio maana wamebarikiwa, ila sasa mmebakia nyie wenzangu na mie mnaoiponda israel na kuishabikia oman, iraq, afghanstan, somalia ndio maana laana na matatizo yamewajaa na sasa mnabakia kulumbana ninyi kwa ninyi.
Sasa Sheikh Ponda kama anajua waislam ni 80% ya watanzania wote, hivi kuna sababu gani ya kutaka kipengere cha dini kiwepo kwenye hizo karatasi za sensa?
Mi binafsi ningependa Waislam wote wogemee hiyo sensa then serikali iendelee na utalatibu wake after that tutajua tu waislam wako wangapi even though hatutajua wakristo pia wako wangapi kwasababu nchi hii ina dini nyingi including wapagani!
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu (Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali kuhesabiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba, inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.
Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wengi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.
"Waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa," alisema Shekh Ponda.
Hivi karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Chanzo: Nipashe
Huyu Sheikh amezipata wapi hizo takwimu kwamba 80% ya Waislamu TZ ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote? Halafu baada ya Sensa ya dini ikajulikana waumini wa dini fulani ndio majority italisaidiaje Taifa? Ninaamini kuwa wapo waislamu wengi Tanzania wasioyumbishwa na kauli na misimamo ya viongozi wao, lakini viongozi wa aina hii wana mchango gani kwenye ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla?
Hivi shetani ana akili kuliko mungu? Haujui shatani atakundanganya ili utekeleze maovu anayotaka?Jini hawezi kuwa above god hata siku moja! Ni mawazo finyu.