Sheikh Ponda aachiwa Polisi kwa dhamana

Sheikh Ponda aachiwa Polisi kwa dhamana

"Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko"
Hili neno la zamani wakati natoa ahadi za chipukizi.
 
Huyo Ponda bila kupewa adhabu kali uchochezi (au kejeli) hawezi acha
Polisi wamekosea sana kumwachia
Siku yakimkuta mama au baba yako ndio utasema haki nimuhimu hats nape hakujuwa kama kunawatu hawataki haki wao ni madaraka tu
 
Huyo Ponda bila kupewa adhabu kali uchochezi (au kejeli) hawezi acha
Polisi wamekosea sana kumwachia
Wewe unataka adhabu gani apewe.
Maana hadi risasi zilimuonja.

Hivi leo mpendwa wetu akipata nafuu akiludi na akijalibu kukosoa walioko juu ambao wewe unawatete bado utashauli adhabu kali itolowe dhidi yake.?
 
Taarifa kutoka Polisi Sheikh Ponda kaachiwa kwa dhamana pamoja na kuwa hakukuwa na sababu ya kumnyima dhamana siku ya jana.

Ikumbukwe kuwa Jeshi la Polisi lilimtaka Sheikh Ponda ajisalimishe Polisi ndani ya siku 3, vinginevyo hatokuwa salama. Baada ya kupata wito wa Polisi, jana Sheikh Ponda aliripoti Kituo Kikuu cha Polisi, asindikizwa na jopo la wanasheria.

Sheikh Ponda alituhumiwa na Jeshi la Polisi kufanya uchochezi kwenye mkutano aliofanya na waandishi wa habari. Zaidi kuhusu mkutano huo soma => KARIAKOO, DAR: Polisi wavamia mkutano wa Sheikh Ponda, wakamata waandishi wa habari wawili baada ya kumkosa Ponda

---------
Sheikh Ponda released from police custody this evening, spokesperson of the Council of Islamic Organisations Sheikh Rajabu Katimba confirms.

Sheikh Ponda Ameachiwa huru jioni ya Leo kutoka Mahabusu. Sheikh Rajabu Katimba Msemaji wa Baraza la Taasisi za kislamu amethibitisha.

CHANZO: The Citizen

Aisee.....
Itabidi akatambike sasa kama alivyosema Wakili wake
 
Sheikh Ponda ukimsikiliza hakika ana maneno kuntu wengi wanamuelewa...

Mwenyezi Mungu mfanyie wepesi katika masahibu yote anayokutana nayo Inshallah.
 

Huo ndio ukweli Ponda ni mchochezi aliye kubuhu
Akifuatiwa na Musa Kundecha, Mohammad Issa, Ally Basaleh na Suleiman Kilemile.

Usimsahau pengo,mzee wa upako,sheikh Zuberi na Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom