Sheikh Mohamed; Sio 'wivu' wa kidini, ni fedha zetu, only | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Mohamed; Sio 'wivu' wa kidini, ni fedha zetu, only

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Jan 17, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Sio Mazoea yangu hata siku moja kuanzisha wala kuchangia topic zinazohusiana na dini. Hata hivyo kwa leo naomba tu nimwambie huyu shehe anayefanya kipindi live pale channel ten (kama sijakosea anaitwa Mohamed, kama nimekosea aniwie radhi) kuwa kati ya hoja zake kumi juu ya mahakama ya kadhi, ni moja tu iliyokuwa sahihi, na ya pili ambayo hakuitaja kabisa.

  Shehe alijitahidi kueleza kisomi sana kuhusu suala kuwa serikali itamlipaje kadhi, ilhali hayupo kwa maslahi ya taifa zima. Hoja yake ni kuwa hata sasa mahakimu wa kawaida (wa serikali), wanaolipwa na kodi za watanzania wote, bado wanahukumu kesi za masuala ya kiislamu (ndoa, mirathi, wakfu, malezi ya watoto) ambayo yanayohisiana na kadhi. Kwa hiyo mwanazuoni huyu anasema kuwa kama wanalipwa mahakimu hawa ambao wanafanya kazi, pamoja na hizi zinazohusiana na dini, then hakuna ubaya wakiwepo wanaohusika na dini (kadhi) peke yake, na bado akalipwa na serikali (kama nilikuelewa vyema, ndivyo ulivyomaanisha mwalimu).

  Hata hivyo pamoja na hoja zako shehe, mi napenda kukujulisha yafuatayo
  1. Hoja kuwa wasio waislamu wanakataa kadhi kwa sababu ya 'wivu' wa kidini, kwangu mimi sio kweli, mi (naamini na wengi wasio waislamu) nakataa kadhi kwa sababu ya kodi yangu.
  2. Hoja yako kuwa mahakimu wa serikali wa kawaida bado wanafanya kazi za kadhi ni sahihi lakini kumbuka hawa hawafanyi tu za kadhi, wanahukumu pia kesi za kimila (kikabila), kiukoo nk. Kama tukisema awepo hakimu (kadhi) anayelipwa na serikali leo, then tutawakataliaje wasambaa wakitaka hakimu wao atakayehukumu kesi zao za kimila? wapare je? wasukuma/ nk.

  Hapa namaanisha kuwa yapo makundi tofauti ya watu humu nchini wenye sheria zao wanazozitambua, hivyo sio busara kila kundi (wakiwemo waislamu), kutaka awepo hakimu specific wa kuhukumu tu kesi zao, na bado alipwe na serikali. Mi nadhani utaratibu wa sasa kuwa kama hakimu wa kawaida hana weledi katika sheria za kundi fulani la dini au kabila, au jingine lolote, then kwa mujibu wa sheria hakimu huyo ana mamlaka ya kuomba ushauri kutoka ndani ya kundi hilo, mathalani masheikh, kwa mfano.

  Serikali itabeba mzigo mkubwa sana kama ikiruhusu kila dini, na kila kundi likawa na taasisi yake inayolipwa nayo.

  Bado hoja ulizotoa sheikh kuwa ni kwanini waislamu wasianzishe mahakama ya kadhi chini ya mamlaka yao wenyewe, eti itakosa authority kwa maana kuwa kunaweza kuwa na makundi tofauti, kwangu hiyo ni hoja dhaifu na inayowadhalilisha waislamu. Sidhani kama taasisi kubwa kama waislamu wanaweza kushindwa kuwa na hierarchy inayoheshmika kiasi cha kuwa na makundi yanayopingana. Sijawahi kusikia kumekuwa na Mufti wakuu wawili Tanzania, je mufti anateuliwa na raisi? Sasa iweje watu ambao wana uwezo wa kuchagua,na kumheshimu kiongozi wa taasisi yao nchini watashindwa kufanya kwa sehemu tu ya taasisi hiyo, yaani kadhi.

  Sheikh Mohamed pamoja na waislamu wote wenye nia ya kushinikiza serikali ikubali mahakama ya kadhi kuwa chombo cha dini kinachoendeshwa na serikali, naomba niwashauri kuwa, kama kweli mnapenda amani ya nchi hii, basi heshimuni dini nyingine na muanzishe hiyo mahakama bila ya kuihusisha serikali, kwa hata dini zingine zimeanzisha taasisi nyingi sana bila kuihusisha serikali, Hakuna sababu ya kuitumbukiza hii nchi katika malumbano yasiyo na msingi, nawaomba ndugu zangu waislamu...
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  cha msingi ni kuanzisha mijadara na matamasha ya viongozi wote wa dini ili kuweka mambo sawa na kupunguza manunguniko ya pande zote
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu tatizo la wenzetu ni kuwa wako very myopic na short sighted badala ya kufanya kazi za kiuchumi na kusoma ili kuondoa ujinga wao wanakazania marumbano yasiyokuwa na tija kwa nchi yetu!
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tuko uko juu, kama huyu Sheikh hataweza kuelewa hoja yako basi anaweza tu kueleweshwa ahera. HATUTAKI TANZANIA YETU IINGIE KWENYE MIGOGORO YA KIDINI KWA MASILAHI YA WACHACHE!

  Tunawaheshimu sana ndugu zetu mnaofuata dini ya kiislamu lakini tunawaomba muachane na ombi la kutaka serikali igharamie uanzishwaji na uendeshwaji wa taasisi yenu ya kidini, hata kama serikali na mkuu wa nchi wako radhi kufanya hivyo. Sisi wenyenchi hatutaki kuingia kwenye mgogoro huu!
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huna hoja pumba tupu.
   
 6. b

  bilabaye Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Zomba, Uhuru wa mawzo unopiganiwa ni pamoja na mawazo yale tusiyopenda kuyasikia, kwenye thread yako umehoji waoneshe pumba, nawe onesha pumba instead of throwing accusation!
   
 7. i

  ibange JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  tuheshimu mawazo ya wengine huo ndio uungwana. unaposema mwenzako hana hoja pumba tu ni upumbavu. mimi nasema kwa vile mahakama ya kadhi ni swala la ibada, kwanini serikali circular itoe pesa za kuendesha ibada? hakutakuwa na mahakama ya kadhi, over our dead bodies! najua kuwa draft ya katiba mpya itakuwa na mahakama ya kadhi na ndio mpango wa jk. ila haitapita trust me. dont underestimate xtians
   
 8. ketwas

  ketwas JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kama wanataka mahakama ya kadhi basi na wakristo watataka mahakama ya kikristo na ambayo yatagharamikiwa na serikali,hata wapagani watadai mahaka yao waanze waonde moto utakaotokea,hadi mahakama ya kimila itahitajika na igharamikiwe na serikali,kwani tutakakokwenda ni kulekule kwa zamani wakati wa mangi mariale alikuwe.....wengine mnawajua waorodheshe......
   
 9. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ni busara tuu, itakayo amua mambo haya, hiyo dini tunajifanya sisi ndo tumeikamata kuliko waarabu wenyewe?
  Umwagaji damu unakaribia
   
 10. L

  Leney JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 315
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Of recent umekua ukiandika post, halafu watu wakikandia, unawaambia wakandie kwa hoja... au sio???
  Basi onyesha mfano... kama wewe unaona ni pumba..prove it by writing your mbolea....

  Jamani lets walk the talk...
   
 11. G

  Godwine JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mbona unapoteza dira ? ha ha ha punguza jazba
   
 12. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu ni unafiki,tungeweza kuanzisha wenyewe lkn tatizo tumegawanyika mno,bakwata hawezi kubali mawazo ya shura ya maimamu and viceversa achilia mbali kuheshimiana,tusaidieni jamani suala la ibada yetu ni mhimu
   
 13. shungurui

  shungurui JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2008
  Messages: 1,587
  Likes Received: 1,557
  Trophy Points: 280
  Hivi wanaogharamia mashehe wanaofungisha ndoa za kiislamu ni nani?
  Hivi serikari ndo iliadhisha utatatibu huu wa kufungisha ndoa kwa niaba ya waislamu?
   
 14. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naishi na m-Irani hapa majuu. Mufahamuvyo wao ndo shina la uislamu. Ni rafiki yangu saaaaaaana, anashauri kama Tanzania imeichoka amani yake waige hayo ya mahakama ya kadhi. Mtavurugana miongoni mwa dini na madhehe bu anuwai, na mwisho wake hata waislamu kwa waislamu watavurugana. Anasifu Tanzania kuwa na ustahimilivu kwa kidini, jambo ambalo Irani hakuna!! na Katika mazungumzo, anasifu muasisi Nyerere (hayati-MUNGU akuweke pema) kuliona hilo mapema na kuweka misingi imara kuwa "SERIKALI HAINA DINI-wananchi wake wako huru kuabudu chochote. Hilo ndo limetufanya tuwe salama muda wote ukilinganisha na nchi zingine. tunaoleana, ndugu wanadini tufauti, tunajaliana,tunashirikiana katika sherehe na majonzi. Haya hayawezi kuwepo kama serikali itaanza changanywa na cheche za dini. Kwa msingi huo, dini yeyote inayo haki ya kuanzisha chohcote ikiaminicho kama taasisi ya kwake, wala si ya serikali-hapo tutakuwa salama.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Leta mchele basi we zoba sijui zomba!
   
 16. M

  Mzalendoo Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kh ndug zangu,mimi ni muislam lakn siku zote siafik wazo la mahakama ya kadh kuw ktk katba,heb tufikirie vzur na tuongozwe na busara zaid,tusije kuw chanzo cha umwagaj dam.
   
 17. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inahitajika elimu ya mkazo sana kwa hawa ndugu zetu waislam,hawatafanikiwa wanachotaka na watabaki kulalamikia mambo ya kipuuzi.Sidhani kama kuna njia nyingine ya kuendesha serekali kwa ufanisi zaidi ya ile ya kutotambua dini huku tukiruhusiwa kuabudu kwa ubinafsi wetu.Katiba inatutambua kama raia wa TZ na kutaja kuwa tunatakiwa kuhudumiwa kwa usawa,sasa hawa waislam hawataki usawa?au hiyo dini yao italeta usawa zaidi kwa watz wote?waache ubinafsi haya mambo wanatakiwa wafikirie kitaifa zaidi na si kwa dini yao tu.Mnao wasomi wengi sana tu embu kaeni nao wawasaidie,acheni kulala lala na kunywa kahawa tu!
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi kule kenya ambako waislam ni wachache (20%) so ndo walitakiwa wakatae kwa sana tu? Mbona wameona logic na ikawepo? Kule south Africa Je? nako ni waislam pekee au ni % ngapi? Na kwengineko kwingi, hebu angalieni kwenye mtandao mtaona. Je waislam ni % ngapi hapa Tz? Si zaidi ya 50%. Je wingi huo wote ni wakupuuzwa?
  halafu pia wewe yaelekea ni kilaza wa hesabu, hebu cheki mfano wa mchanganuo huu hapa chini
  hakimu1-----kesi za kawaida 20+za mambo ya waislam 5 ======25
  hakimu2------ 20+ 5=======25
  hakimu 3------ 20+ 5=======25
  hakimu 4----- 20+ 5=======25
  Hakimu5----- 20+ 5=======25
  -----------------------------------------------------------------------------------
  Total 100 + 25=======125

  kama uwezo wa hakimu ni kuhukumu kesi 25 mathalani kwa mwezi na katika kesi hizo zipo 5 ambazo kadhi alitakiwa kuzitenda, why don't we have professional kuliko kuwa na mtu wakubahatisha mara awaite mashehe nini! ubabaishaji mtupu. Hivi mnasema eti na wakristo nao waanzishe zakwao, kwani wao wanasheria? kuna nchi ngaki zenye wakristo karibia wote nitajieni ni nchi gani inaongozwa kw sheria zake? nchi zenye waislam je? kenye mbona kuna mahakama ya kathi kwani nini kawaanzishi hizo za kikrsto tuzione? hawa si jirani zetu kwanini tusijifunze kutoka kwao?
  Hivi kama wakoloni waliona ni muhimu kwa waislam kuwa na mahakama ya kadhi imekuwaje waTz wenzetu hawaoni umuhimu huo. NA SEMA HIVUI HUU NI UNAFIKI, NA NI WIVU WAKIDINI. PERIOD!
   
 19. Q

  QALQAL MARTIN Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dini ni ya mwenye dini, misikiti na mahakama za dini itajengwa na wenye dini! Na cvinginevyo wakati cc tunajadili mambo yacyo na maana wenzetu wako mwezini(outerspace) wengine wako hata hapa tz wanachota madini,wanatalii mbuga zetu booking wanafanyia kwao? DINI YA KWANZA NI NCHI YAKO, enyi vichwa veusi acheni utumwa wa imani na akili ni aibu kijana mweusi kujiita KIJANA KIAARABU na maanisha "AL-Shabab"
   
 20. m

  mananasi Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakristo kama wana mfumo wao wa mahakama basi kheri na tuuone. Lakini kama ni mambo ya kuunda unda tu kwa kuiga na kuona kwanini waislamu wana mahakama yao basi na sisi tuanzishe yetu, haitoweza kudumu. Kwanza kama ni kitu wanakiunda basi itabidi kwanza wakakijaribu isije ikawa maafa katika mambo ya kuamua haki. Kwa upande wa waislamu, mahakama ya kadhi haina shaka ndani yake, mbali ya kuwa imeletwa ready made kwa binaadamu kutumia kutoka kwa yule aliyetuleta hapa duniani, lakini pia mifano hai ya mafanikio yote haihesabiki katika nchi mbali mbali duniani. Wala si lazima serikali ikalipia uendeshaji wa mahakama ya kadhi, hata waislamu wenyewe wanawezwa kutozwa kama kodi ya mahakama ya kadhi kwa ajili ya kuiendesha.
   
Loading...