GE2025 Sheikh Kaniki: Siasa na dini havitenganishiki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,716
Reaction score
2,746
Sheikh Ibrahim Kaniki amesema hakuna utengano kati ya dini na siasa, akisisitiza kuwa masuala ya kisiasa huathiri moja kwa moja maisha ya waumini wa dini, hivyo ni muhimu viongozi wa dini kushiriki katika kuombea amani, haki na viongozi wanaokumbwa na changamoto.

Akizungumza siku ya Jumamosi baada ya kuongoza dua maalum kwa ajili ya kumuombea heri na ulinzi Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, aliyeko rumande kwa tuhuma za uhaini na uchochezi, Sheikh Kaniki amesema:

“Ukisema siasa haihusiani na dini unakosea sana… ni sawa na kusema kwa sababu mimi ni mtu wa dini sitanunua, sitauza, sitakwenda hospitali, nitakuwepo tu – hiyo itakuwa balaa”.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA Tawi la Gongo la Mboto, Deus Kato, amesema ni siku 100 sasa tangu Tundu Lissu awekwe rumande kwa makosa aliyoyaita ya ‘mchongo’ huku akisema kuwa kilio cha wanachama wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla kimefikishwa kwa Mwenyezi Mungu kupitia dua hiyo, akibainisha kuwa kilio hicho hakiwezi kufumbiwa macho.

Nao Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), kupitia Mwenyekiti wake Wakili Deogratius Mahinyila, walishiriki ibada hiyo ya Kiislamu, wakisisitiza kuwa dua ni silaha halali kwa wanyonge wanaotafuta haki.

Dua hiyo imefanyika katika kata ya Gongo la Mboto, wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam ikiongozwa na masheikh mbalimbali na kuhudhuriwa na wanachama wa CHADEMA, wafuasi wa dini ya Kiislamu, na wananchi wa kawaida.

Source Jambo TV

View: https://www.youtube.com/watch?v=4wXfohDPUt8
 
View attachment 3420218
Source Jambo TV

View: https://www.youtube.com/watch?v=4wXfohDPUt8

siasa ni maisha yako maana utahoji kuuliza haki yako hapa naona watu wanaanza kuelewa sasa
 
Back
Top Bottom