PreGE2025 TANZIA Sheikh Jabir Haidar akutwa amefariki Bumbwisudi, chanzo cha Kifo bado kitendawili

PreGE2025 TANZIA Sheikh Jabir Haidar akutwa amefariki Bumbwisudi, chanzo cha Kifo bado kitendawili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mwili wa Sheikh Jabir Haidar Al Farsi umekutwa usiku wa kuamkia leo, Jumatano Mei 28, 2025, katika eneo la Bumbwisudi akiwa tayari amefariki dunia. Taarifa za awali zinaeleza kuwa huenda marehemu alishambuliwa na watu wasiojulikana, ingawa pikipiki aina ya Vespa aliyokuwa akiitumia ilikutwa pembeni yake ikiwa haijaharibika.

1748433387723.png
Hadi sasa chanzo halisi cha kifo chake bado hakijafahamika rasmi, na uchunguzi unaendelea. Maziko ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo hii Jumatano.

Kwa upande wa wanawake yatafanyika nyumbani kwa kaka wa marehemu, Kassim, huko Kikwajuni, na kwa upande wa wanaume msiba utaswaliwa Msikiti wa Ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.

1748433647153.png
=======​
Wakati mwili wa Sheikh Jabir Haidar Jabir ukiokotwa ukiwa umetelekezwa, polisi wamesema haujakutwa na majeraha yoyote huku mazingira ulikokutwa hayakuonesha dalili zozote za vurugu, hivyo inawezekana alipata madhara sehemu nyingine na kupelekwa katika eneo hilo.

Akizungumza leo Jumatano Mei 28, 2025 na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Richard Mchomvu amesema jana saa 5:00 usiku, Kituo cha Polisi Bububu kilipokea taarifa ya kuokotwa kwa mwili wa mwanaume maeneo ya Kizimbani.

Amesema baada ya kupata taarifa hiyo, Kaimu Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Magharibi A, alifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili huo.

"Kaimu wa upelelezi alifika eneo la tukio na kufanya upelelezi wa awali na alipata kitambulisho kilichomtambulisha kwa jina la Jabir Haidari Jabir na aliuangalia mwili haukuwa na jeraha lolote," amesema Mchomvu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Richard Thadei Mchomvu akitoa taarifa kuhusu kuokotwa kwa mwili wa Sheikh Jabir Haidari Jabir leo Jumatano Mei 28, 2025 ofisini kwake Madema.

Kwa mujibu wa Kamanda Mchomvu, mazingira ulikokutwa mwili huo hayakuonesha dalili zozote za vurugu, hivyo ieleweke kuwa pengine alipata madhara sehemu moja na kupelekwa eneo hilo.

Amesema, mwili huo ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Amesema Jeshi la Polisi lilibaini kuwa marehemu alikuwa mkazi wa Fuoni na walikuwa wakiishi wawili yeye na kijana aliyekuwa akimsaidia kazi.

Mchomvu amesema, walipogundua kuwa ni mkazi wa Fuoni walifanya uchunguzi wa awali na walitambua alikuwa anaishi na kijana wa kazia, hata hivyo hakumtaja jina.

Amesema jana Mei 27, 2025 saa 12:00 jioni sheikh huyo alitembelewa na kijana ambaye alionesha kufahamiana naye na walikaa kwa muda sebuleni wakizungumza wakati huo kijana wake wa kazi alikuwa ndani.

"Jabir alizungumza na kijana huyo kama nusu saa wakatokea watu wengine watano ambao walijiunga pamoja na ilipofika saa 2:30 usiku waliondoka naye, kabla ya kutoka hausiboi alimuuliza anakokwenda, akamjibu kuwa atamjuza baadaye hivyo haikufahamika anakwenda wapi hadi mwili wake ulipookotwa,” amesema.

Hivyo, Kamanda amesema mpaka sasa chanzo cha kifo chake bad hakijajulikana.

“Na bado haijafahamika watu alioondoka nao wako wapi na sisi bado Jeshi la Polisi linapambana kufuatilia tukio hilo,” amesema kamanda huyo.

Amesema jeshi hilo linaendelea kufanya upelelezi ili kubaini alioondoka nao walienda wapi, alikufaje na kwa nini mwili wake ulikutwa maeneo hayo.

"Nataka kuwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwa hatua ambayo tumeifikia tutawajua walioondoka naye na kitu kilichotokea, najua kuna minog'ono mingi mtaani ila hayo ndio yaliyopo mwili haukukutwa na jeraha lolote," amesema Mchomvu.

Naye mtoto wa kaka wa marehemu, Mudthir Kassim Haidar amesema wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko kwani jana aliondoka kwao na kwenda kwake akiwa mzima licha ya kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu na moyo lakini jana alikuwa salama.

“Jana baada ya kupata taarifa zinadai ameuawa kwa kupigwa lakini tunachokijua alitoka nyumbani akiwa mzima na amewasiliana na watu akiwa salama. Suala la kuwa ameuawa tunasubiri na kuwaachia jukumu hilo Polisi kama ameuawa au imekuwaje, wao ndio watatoa taarifa,” amesema.
Pia soma:
~
Sheikh Jabir Haidar akutwa amefariki Bumbwisudi, chanzo cha Kifo bado kitendawili
~ Zanzibar: Watuhumiwa Sita wa Mauaji ya Sheikh Jabir Haidar Jabir wapelekwa rumande
 
Kwa hiyo sasa wamehamia upande ule mwingine?
Mwili wa Sheikh Jabir Haidar Al Farsi umekutwa usiku wa kuamkia leo, Jumatano Mei 28, 2025, katika eneo la Bumbwisudi akiwa tayari amefariki dunia. Taarifa za awali zinaeleza kuwa huenda marehemu alishambuliwa na watu wasiojulikana, ingawa pikipiki aina ya Vespa aliyokuwa akiitumia ilikutwa pembeni yake ikiwa haijaharibika.

Hadi sasa chanzo halisi cha kifo chake bado hakijafahamika rasmi, na uchunguzi unaendelea. Maziko ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo hii Jumatano.

Kwa upande wa wanawake yatafanyika nyumbani kwa kaka wa marehemu, Kassim, huko Kikwajuni, na kwa upande wa wanaume msiba utaswaliwa Msikiti wa Ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.

Mwili wa Sheikh Jabir Haidar Al Farsi umekutwa usiku wa kuamkia leo, Jumatano Mei 28, 2025, katika eneo la Bumbwisudi akiwa tayari amefariki dunia. Taarifa za awali zinaeleza kuwa huenda marehemu alishambuliwa na watu wasiojulikana, ingawa pikipiki aina ya Vespa aliyokuwa akiitumia ilikutwa pembeni yake ikiwa haijaharibika.

Hadi sasa chanzo halisi cha kifo chake bado hakijafahamika rasmi, na uchunguzi unaendelea. Maziko ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo hii Jumatano.

Kwa upande wa wanawake yatafanyika nyumbani kwa kaka wa marehemu, Kassim, huko Kikwajuni, na kwa upande wa wanaume msiba utaswaliwa Msikiti wa Ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.

Wivu wa kimapenzi, Vespa na wadada damdam.
 
Back
Top Bottom