tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,838
- 18,250
Shehe huyu kutoka msikiti wa Madina ambao haukuweza kujulikana mara moja mkoa ulipo, amesikika akiongea kwa ukali sana akiwananga wale wote wanaomtukana mama kwa sababu ya kuuza bandari kwa waarabu. “Hawa waarabu wamekuja kuchukua bandari yao waliyoijenga mwaka 1896 kinawauma nini?” Ameuliza.
Shehe ameenda mbali zaidi kusema kwamba kipindi cha serikali ya Magufuli watu walikuwa kimya kwa sababu mtu yeyote aliyejitokeza kusema aliuawa na pia kuna baadhi ya wanasiasa waliikimbia nchi kwa kuhofia kuuawa.
Nisimalize utamu, hebu msikilize shehe wewe mwenyewe kwenye klipu hapo chini.
MAONI YANGU
Huyu shehe namkubali lakini kitendo chake cha kuchanganya suala la kisiasa na uislamu sio vizuri. Hata kuifananisha serikali ya Magufuli na hii ya Samia kisa tu Samia ni muislamu na Mafuguli ni mkristo, ni suala lisilopendeza hata kidogo. Yeye angejikita tu kwenye hoja ya msingi bila kuingiza udini.
Nawasilisha.