She wasn't a girl ...................wasn't yet a woman

KIKUNGU

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
845
585
Good friday guys and i wish you an enjoyable weekend as well.Jamani nina kisa hiki nataka ku-share na nyinyi na naomba experience zenu hasa kwa wale ambao ni vijana/wadada wa 90's au mapema 2000.Naomba mchangie ili tuwape experience wale ambao either wanatarajia au karibuni wameoa/olewa,hasa wewe BABU DC,the BOSS,ASHADII na wengineo wote na wewe LIZZY hata sijui uko wapi maana umeadimika.
Ilikuwa mwanzoni mwa karne hii nilkuwa vacation hapa nyumbani nikiwa nimemwacha mchumba wangu(my high school sweetheart) ughaibuni,nilikutana na dada wa kibondei(kabila moja kule Tanga),tulikuwa tunasali nae kanisa la St Anthony kule Chumbageni.Ni ajali iliyotukutanisha,kilikuwa ni kipindi cha mwezi wa dec,nikiwa kanisani,joto kali,msongamano wa watu na mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa toka baridi ya winter na joto kali la dec hapa nyumbani,nilianguka nikazimia kanisani.Nilikuja zinduka nikiwa Tumaini hospital pembeni yangu kuna mdada,she was a really lady in every sense.Kwa wale mnao wajua au kusikia hawa wabondei ni kama mchanganyiko wa wabantu na waarabu.Akaniambia kwa nini niko pale na kwamba ni yeye alinileta pale kutoka kanisani kwenye gari la mama yake.Nilitoka hospital baada ya DR aliyekuwa ananihudumia kuniambia sikuwa na tatizo.
Haikuwa coincedence,lakini zilikuwa siku zangu za ujana na nilikuwa sijaoa japo nilikuwa na mchumba,lakini kwa maoni yangu unahitajika "KU-PLAY AROUND" kabla ya kuoa,but try to play safe,if you know what i mean.Niliingia kwenye mahusiano ya muda mfupi ni huyu binti.Katika kufahamiana,yeye ndio kwanza alikuwa amemaliza form six pale Kifungilo girl's secondary, Lushoto.Alinipagawisha kwa muda mfupi tuliokuwa pamoja.Na kwa kuwa tulikuwa bado tuna "ISSUES" za ku sort out na mchumba wangu wa ughaibuni,mawazo yalibadilika,seriously nilitaka kutangaza uchumba na huyu binti wa kibondei.
My mother(mungu amrehemu huko aliko)stepped in,aliniambia kuwa huyu siwezi kumuoa sababu hakuwai kuniambia mbaka mungu lipomchukua.Yule dada nae hakuwa tayari kukubali uchumba wangu kwa sababu alikusema bado yeye ni binti na bado hajafikia umri wa kuolewa kwa kipindi cha miaka mitano iliyofuata japo mama yake alibariki mahusiano yetu kwani sikuyaficha kwao.
Two years later nilimuoa my high school sweetheart,kanisani pale pale nilipoanguka two years ago,yule binti akishuhudia nikiwa altareni.Yule binti niliendelea kuwasiana nae japo siwahi kurudi tena bongo mpaka kipindi naoa,na yeye alikuwa mwaka wa pili chuo kikuu.Alimaliza chuo akapata kazi ya ualimu wa secondary huko huko Tanga.Alikutana na Engineer mmoja wa Tanesco ambae alikuwa ni either age mate wangu au mkubwa kunizidi.Four years later yule Engineer alifariki na yule dada miaka miwili baadae,kwa huu ugonjwa wa kisasa.
Ten years later with two lovely kids, i divorced my wife,kwa sababu ambazo ni aibu kuzielezea hapa.
Miaka yote iliyobaki ya maisha yangu nitaendelea kujiuliza (regretting),japo michango yenu nitaipa utmost consideration kwamba,kwa kuanguka kwangu kanisani na kukutanishwa na yule binti yalikuwa ni mapenzi ya mungu ili mimi nimuoe yule binti labda ningekuwa bado nafurahia maisha ya ndoa na watoto wangu?Wazazi wana nafasi gani ya ku play kwenye maamuzi ya yupi watoto waoe?Have you played around before getting married and what is/was your experience?Je kuna ukweli kwamba kuna makabila hayafai kuoa(take this as reference,kwamba wabondei wanaitwa "MLANGO WA NANE",kwamba ni wachoyo kidogo,wachawi kidogo,malaya kidogo, yaani wana vitu vibaya vinane kama hivyo hapo).Kwamba labda yule binti kama ningemuoa labda asingekutana na yule Engineer ambae alimpa kale kaugonjwa?
Naomba michango yenu na sio lazima uongelee kila kitu,unaweza kuchagua kitu kimoja ukachangia.

Mbarikiwe sana
 
FATE................. !!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Not binding her in wedlock was your blessing. Everything happens with a reason. Even your divorce could be a blessing.

Pray to your lord for being alive and well. Give thanx to your creator for leading you in an open and free path.

Good luck in your future. (Bondei girls are pretty) It is not true what you said of them.
 
'Ninge. . .'
Pole aisee
I believe in destiny, huna cha kujilaumu
Ndo maisha yalivyo
Songa mbele, na jaribu kupigania furaha yako.

Japo sikatai kwamba kuna experience ambazo zinaacha mioyo ikiwa na makovu makubwa na hayasahauliki kirahisi.
 
Maisha hayana formula, ni ngumu kupredict aisee. Cha msingi mshukuru Mungu kwa nafasi ya kuwa hai na familia uliyonayo kwa sasa. Jitahidi kusahau yaliyotokea na concentrate kwenye kuitunza familia yako na kuelea kwenye malezi mema ya kumcha Mungu.

All the best.
 
FATE................. !!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Not binding her in wedlock was your blessing. Everything happens with a reason. Even your divorce could be a blessing.

Pray to your lord for being alive and well. Give thanx to your creator for leading you in an open and free path.

You are right Doctorz and thanks for your views.The "MLANGO WA NANE" issue is not my views,ask any one coming from Tanga will tell you,even themselves knows it.Bondei ladies?woooh get to know them,really beauty
 
'Ninge. . .'
Pole aisee
I believe in destiny, huna cha kujilaumu
Ndo maisha yalivyo
Songa mbele, na jaribu kupigania furaha yako.

Japo sikatai kwamba kuna experience ambazo zinaacha mioyo ikiwa na makovu makubwa na hayasahauliki kirahisi.

Asante sana Kongosho,that is what am doing.Mungu akubariki sana.Nipe basi experience yako kama umeolewa/ao au kabla
 
Maisha hayana formula, ni ngumu kupredict aisee. Cha msingi mshukuru Mungu kwa nafasi ya kuwa hai na familia uliyonayo kwa sasa. Jitahidi kusahau yaliyotokea na concentrate kwenye kuitunza familia yako na kuelea kwenye malezi mema ya kumcha Mungu.

All the best.

Asante Horsepower,mungu akubariki sana.Nipe kauzoefu kako eitherway
 
1.Tabia ni tabia tu, haitegemei sana kabila la mtu. Huko wanakosema hakufai unaweza kupata mwenzi safi kabisa
2. Kanisani ulidondoka kwa ugonjwa au mapepo?
3. Mzazi anaweza kupendekeza umuoe nani hasa mtu mwenyewe anapotoka maeneo anayoishi mzazi.
4. Zaidi ya hapo use your sisters. Kama una dada yako mlieshibana, muintroduce kwa wifi yake ili kama ana maoni
aseme. Utashangaa mara nyingi hawakosei, atakujibu huyu sawa au hakufai.
 
mkuu kwanza nikupe pole!mimi ni "mtabiri wa mambo ambayo yangetokea"!!!!natabiri kwamba yule dada wa kibondei yeye ndio kamuambukiza ugonjwa yule engineer!natabiri kwamba ungemuoa yule dada wa kibondei ungekuwa umechukua nafasi ya engineer,ungekuwa umeambukizwa,ungekuwa umeshakufa,usingeandika post hii,nami nisingechangia hapa!.....so be happy now...kila jambo hutokea kwa sababu,amini...ulichonacho ndio kitu bora zaidi Mungu amependa kukupa!nenda kwa amani
 
Mc Tilly u have said it all, the secret behind all success is appreciating where the life is taking you. Believe that all that has happened to you were meant to be so for your betterment and you will be overwhelmed with blessings Kikungu.
 
......Miaka yote iliyobaki ya maisha yangu nitaendelea kujiuliza (regretting),japo michango yenu nitaipa utmost consideration kwamba,kwa kuanguka kwangu kanisani na kukutanishwa na yule binti yalikuwa ni mapenzi ya mungu ili mimi nimuoe yule binti labda ningekuwa bado nafurahia maisha ya ndoa na watoto wangu?Wazazi wana nafasi gani ya ku play kwenye maamuzi ya yupi watoto waoe?Have you played around before getting married and what is/was your experience?........

Ungemuoa huyo binti usingekua na hao watoto ulionao sasa....LABDA ungekua na watoto wengine...labda usingekua na watoto....labda huyo binti ndo alipeleka hako kaugonjwa kwa jamaa....

fate mazee.....no regrets, history wont change!
 

Ungemuoa huyo binti usingekua na hao watoto ulionao sasa....LABDA ungekua na watoto wengine...labda usingekua na watoto....labda huyo binti ndo alipeleka hako kaugonjwa kwa jamaa....

fate mazee.....no regrets, history wont change!

I wanted to say something like this, lakini nikakosa maneno mazuri. Sure it could have been WORSE! live life to the fullest with no regrets later!
 
kaunga nimefurahi kuona upo........................mie siwezi kuchangia kwa sababu ni wa sixtees.............
 
kaunga nimefurahi kuona upo........................mie siwezi kuchangia kwa sababu ni wa sixtees.............

So una maana in sixtees ndio ulikuwa rijali, nafikiri Kikungu alivyosema wale wa 90s alimaanisha ambao walikuwa in their 20s!

Changia bana, hata kama ni kibabu! LOL
 
I wanted to say something like this, lakini nikakosa maneno mazuri. Sure it could have been WORSE! live life to the fullest with no regrets later!
mmmh zote ni assumption tu maybe hali ingekuwa nzuri zaidi je?
kweli future is unpredictable jamani? kwanini Mungu sometimes anakuwa kimya hivo?
 
Kila linalotokea kwenye maisha lina sababu nyuma yake,kila likuepukalo lina heri na wewe, Tushukuru kwa yote maana ni mpango wa Mungu.
 
mmmh zote ni assumption tu maybe hali ingekuwa nzuri zaidi je?
kweli future is unpredictable jamani? kwanini Mungu sometimes anakuwa kimya hivo?

It is very true, lkn what good can it do tukimsaidia kujutia maamuzi yake ya nyuma?
Every decision has a consenquense, ingawa zaweza zidiana. Kuna series moja ninaiangalia unaitwa "day break"; inahusu jamaa anae experience déjà vu; ameiishi siku moja over and over again, na anapojaribu kubadilisha machaguo bado anakutana na kitu kibaya mwishoni, au mpenzi wake auwawe au dada yake au rafiki zake au yeye mwenyewe afungwe etc.

So my bro alimuoa mkewe, na kumuacha binti wa kitanga; who knows (kama wadau walivyosema), angekuwa yeye ndio kaupata huo ugonjwa si na kaka yangu angeambukizwa?

My bro met his lover wakati hawakuwa vizuri na mchumba wake; so it was only natural kuona kuwa new girl is superb. Angepata nafasi ya kukaa naye kwa muda mrefu kama alivyokaa na mchumba wake huenda asingemuona a saint kivile; who knows.

So Smile dear, kumbatia kila day na u-count your blessings kwani hakuna kitu smooth (happily ever after) labda kwenye fairly tales tu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom