She is having my baby, I can't get married to her!

Huyu binti ni 'mchaga'

Huyu binti,alijifungua mtoto a kike,mtoto sasa ni mkubwa kwa 3yrs,sasa imefika mahala nahitaji kuendelea na maisha yangu AMEKUWA MBOGO

Sikuwahi kuishi nae,na wala kushirikiana nae baada ya ile mimba.Na sikuwahi kutoa ahadi za ndoa pale,lakini AMEKUWA MKALI nilipomwambia sasa ninaendelea na maisha yangu nina mchumba na ninahitaji kuoa.

Amenitishia kuniletea vurugu ofisini,sasa mimi inanisumbua kichwa.ilifika mahala nilitamani nihame dar.

TAFADHALI
Kwanza pongezi kwa kumkubali mtoto. Kinachonishangaza lakini ni kuwa tangu mtoto amezaliwa na kufikia umri huo hamkuwahi kushirikiana naye katika tendo la ndoa. Ulitunza mtoto, lakini uliishi kivyako naye kivyake. Sasa leo unataka kufunga ndoa kwa nini awe mbogo wakati uhusiano wa mapenzi ulishavunjia zaidi ya miaka 3? Ni ajabu hii! Au unatufunga kamba uliendelea kufaidi!?

Kama unayoyasema ni kweli, basi ujue hata kama mzazi mwenzako anang'aka si kwa sababu anakupenda kwani mlishaachana siku nyingi. Ana wivu wa kimaslahi - anataka pesa/mali yako, uendelee kumhudumia yeye na mtoto wenu. Ukioa anaona mali yote atakumbatia mkeo.

Sasa ufanyeje? NENDA kafunge ndoa yako na umpendaye kwa moyo wa dhati. Hata akileta fujo hatafanikiwa kukuzuia kufunga ndoa kwani ni haki yako msingi. Sheria inakulinda.

Ila mtoto usimtelekeze. Endelea kumtunza kama mwanzo. Hapo unawajibika. Vinginevyo utachukuliwa hatua.
 
Kulazimwisha kivipi kwani hiyo mimba ilitunga vipi kama mlikuwa hampendani?? Ikiwa kama ulikuwa humpendi basi wewe ni mbakaji maana hadi mimba itunge ni kwamba ulikuwa unampenda kwa dhati na hukujali kutumia condom, sasa kwanini sasa useme humpendi???

Unajua wewe ni mtu mzima unajua jinsi ya kujikinga sio tu na mimba hata magonjwa ya zinaa sasa kanini ufanye bila kondom.
Huyu binti anahaki kabisa ya kuolewa na wewe mlipendana now unamwona si mali kitu unataka kumtosa. Kwanza unatakiwa umshukuru na kumweshimu maana bila yeye usingeonekana ni rijali na unauzazi ,kwa maoni yangu kumwoa na kuishi nae ni wajibu wako.
Nyie ndio mnao ongeza idadi ya watoto wa mitaani duniani,jambo jingine geuza upande wapili ungekuwa ww umefanyiwa hivyo ungejisikia vipi. tatu angekuw mwanao ama dada yako kafanyiwa hivyo unefurahia!

Ukipata majibu ya maswali nilio kuuliza utajua uchungu alionao huyo dada.
NENDA KAMUOWE ACHA KUONGEZA IDADI YA WATOTO MITAANI NA WSIO NA MALEZI YA PANDE MBILI.

Hayo mawazo potofu ambayo sikuyategemea kutoka kwa borntown, nani asiyejua mitego ya watoto wa siku hizi, isitoshe usifikiri kila mtu anaamini condom, usione ajabu jamaa alimdaka kisimani tia maji tia maji mtoto akajiachia uchochoroni mzee akakosha rungu. Watoto wa kike wanatega sana hasa akijua uko responsible.

Mi nakushauri mpe laivu hata sheria kaka inakulinda...we uliona wapi mtu analazimisha mapenzi, suala la kuwa na mtoto nae si kigezo muhimu, kama vipi chukua mtoto wako na yeye atambae zake. Si anaogopa mzigo sasa kumbe? Hao ndo wale wanawake wanaishi kwa kutegemea wanaume usione ajabu akipata dau kubwa analala mbele. ACHANE NAE MKURU.

Ushauri: tuache kudonoa doa bila mpango maisha magumu litakufikia ooh.
 
Huyu binti ni 'mchaga'

Huyu binti katika ujana ujana ule ilitokea akaconceive

Huyu binti alitaka kutoa mimba nikamsihi sana asifane hiyo dhambi,nilimwahidi kwamba nitamlea mtoto,HILO TU!

Huyu binti,alijifungua mtoto a kike,mtoto sasa ni mkubwa kwa 3yrs,sasa imefika mahala nahitaji kuendelea na maisha yangu AMEKUWA MBOGO

Sikuwahi kuishi nae,na wala kushirikiana nae baada ya ile mimba.Na sikuwahi kutoa ahadi za ndoa pale,lakini AMEKUWA MKALI nilipomwambia sasa ninaendelea na maisha yangu nina mchumba na ninahitaji kuoa.

Amenitishia kuniletea vurugu ofisini,sasa mimi inanisumbua kichwa.ilifika mahala nilitamani nihame dar.

Najua nilikosea,lakini pia sio rahisi kulazimisha kuishi na mtu ambae humpendi,kwa sababu sitakuwa mwaminifu kwake,na hata akilazimisha tutakaa nusu mwaka tu then tutaachana.

waungwana mnisaidie nimweleweshe vipi huyu mzazi mwenzangu kwamba mapenzi hayalazimishwi?

TAFADHALI

Bro haya ndiyo matokeo ya kumdanganya mwanamke unampenda ili mradi ulale nae. Au mli kubaliana tokea mwanzo kuwa it will only be a casual thing? To say the truth umefanya a big mistake on your part. Kama unajua hautaki mtoto why didn't you have protected sex with her? Mkuu kwani haujui matokeo ya kufanya mapenzi ni nini? It's not good to sleep around with someone if you do not love them and this is the result. It's sad that this is what we do to our women. Anyway just to be fair nitai chukulia that maybe you guys only planned to have sex with no strings attached or you just wanted to be friends with benefit. If that is the case you shouldn't have practice the sex married couples engage in. My advise is take the baby. Kama kweli hautaki kumuoa mchukue mtoto. Wanawake wengi hawapendi mapenzi mfanye wote kisha mzigo umuachie mwenyewe. Najua ukimuambia you will take the baby she will leave you alone because she knows she won't have to handle all the expenses. Also allow her full visitation rights. Kaka angu do the right thing.
 
Hivi nyie vijana mnacheza na mama wa watoto zenu sana. Kumbuka kuwa huyo mwanamke akikulaani kaka yangu laana inakupata tena sana tu.
Am talking through experience kaka yangu wa damu alimzalisha mwanamke akamuacha akaenda kuoa kwingine, kilio cha mtoto,mama mtoto na laana zake,mpaka leo kaka yangu na mkewe ndoa haina amani na wifi yangu miaka 7 sasa mimba hapati.wamezunguka dunia nzima kwa madoctor,makanisani na kila pembe, mtoto hawapati.
usidhani huko unakokimbilia ni kwema, utakuja juta baadae. Mrudie Mungu wako then wewe na huyo mzazi mwenzio mrekebishe matatizo yenu.

Funda ndoa endapo tu, mama mtoto wako ata ridhia otherwise jiandae kwa balaa
 
wewe bwana una mkatatizo unauliza swali gani? we huoni huyo ni mkeo tayari?watu wengine bwana!!
 
wewe bwana una mkatatizo unauliza swali gani? we huoni huyo ni mkeo tayari?watu wengine bwana!!

Mkuu mbona upo nje ya mada kabisa. Mke wake kivp sheria inasemaje soma maelezo yake then angalia sheria inasemaje unavyo mbebesha kuwa ni mke wake.
 
Hivi nyie vijana mnacheza na mama wa watoto zenu sana. Kumbuka kuwa huyo mwanamke akikulaani kaka yangu laana inakupata tena sana tu.
Am talking through experience kaka yangu wa damu alimzalisha mwanamke akamuacha akaenda kuoa kwingine, kilio cha mtoto,mama mtoto na laana zake,mpaka leo kaka yangu na mkewe ndoa haina amani na wifi yangu miaka 7 sasa mimba hapati.wamezunguka dunia nzima kwa madoctor,makanisani na kila pembe, mtoto hawapati.
usidhani huko unakokimbilia ni kwema, utakuja juta baadae. Mrudie Mungu wako then wewe na huyo mzazi mwenzio mrekebishe matatizo yenu.

Funda ndoa endapo tu, mama mtoto wako ata ridhia otherwise jiandae kwa balaa

Kweli kabisa. Amejilaani huyu shauri yake.
 
Ongea na watu wake wa karibu, bila shaka wanaelewa mahusiano mliyokuwa nayo kisha utapata nafasi ya kuzungumza nae ili myamalize 'kiutu uzima'. hakuna linaloshindikana. mbaya kurudia makosa. uwe na amani tu ndugu.
 
am telling you by then,i never had any plan!NEITHER A NOR B.nisingependa kuelezea kilichotokea kwakweli kwasababu..................dah!anyaways,AHSANTE KWA USHAURI!the thing is I DON'T LOVE HER!I have tried to in so many ways lakin IT NEVA WORKED

Mkuu Geoff;

Pole sana... Haya ni mazao ya kufanya mambo mengi ya ujana bila kuangalia madhara yake baadae!! hauko pekee ni wengi ila wewe umekuwa gentleman enough kumkubali mtoto, wengine hukataa hata watoto wao.

Ushuri wangu ni kwamba umpe ukweli, mhakikishie future support na uwe firm kwenye maamuzi yako ili mtoto asiteseke... HIli la kuharibiana kwangu naona ni kwa wote na si kwako tu kwani mlifanya mliyofanya kwa hiyari na mambo ya ujana

Please secure your kids future and communicate your way forward firmly so that you enter a next step in life
 
Huyu binti ni 'mchaga'

Huyu binti katika ujana ujana ule ilitokea akaconceive

Huyu binti alitaka kutoa mimba nikamsihi sana asifane hiyo dhambi,nilimwahidi kwamba nitamlea mtoto,HILO TU!

Huyu binti,alijifungua mtoto a kike,mtoto sasa ni mkubwa kwa 3yrs,sasa imefika mahala nahitaji kuendelea na maisha yangu AMEKUWA MBOGO

Sikuwahi kuishi nae,na wala kushirikiana nae baada ya ile mimba.Na sikuwahi kutoa ahadi za ndoa pale,lakini AMEKUWA MKALI nilipomwambia sasa ninaendelea na maisha yangu nina mchumba na ninahitaji kuoa.

Amenitishia kuniletea vurugu ofisini,sasa mimi inanisumbua kichwa.ilifika mahala nilitamani nihame dar.

Najua nilikosea,lakini pia sio rahisi kulazimisha kuishi na mtu ambae humpendi,kwa sababu sitakuwa mwaminifu kwake,na hata akilazimisha tutakaa nusu mwaka tu then tutaachana.

waungwana mnisaidie nimweleweshe vipi huyu mzazi mwenzangu kwamba mapenzi hayalazimishwi?

TAFADHALI

naona kama tunauelewa tofauti, kutokana na ulivyoeleza hapa huyu binti baada ya mimba hukuwahi kukutana naye inamaana ni zaidi ya miaka 3 huna mahusiano naye ya kimapenzi, unavyosema mbogo ina maana anataka kuolewa au nataka assuarance ya mtoto! nahisi huyu binti wala hajawa mbogo kwa kutaka kuolewa nawe ila inawezekana ni kwa kutaka uhakika wa kutunziwa huyu mtoto, na anahaki ya kufanya hivyo, fuata sheria muandikishiane na muwashirikishe wazee ili apate uhakika huo na sidhani kama atakusumbua, sidhani kama anakupenda wala hana haja nawe haiwezekani akupende akae miaka yote hiyo asishughulike na wewe!!! WANAUME BWANA hawaishi kusingizia wanawake pale wanapokuwa wanakosea huna sababu ya kumsingizia huyu binti analazimisha mapenzi,

na kwa maelezo yako kuwa mtoto kampleka moshi inaonyesha huyu binti ni muelewa na anajua anachokifanya maana kwa wanaume walivyo ungemwambia kama issue ni mtoto basi namchukua nitamlea, na anaelewa mlezi wa mtoto ni mama!! nadhani unatafuta kukwepa fuata sheria mtoto umpe haki yake!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom