Wakuu vipi kwema,, simu tajwa hapo juu nimeona nikaipenda sana,, ina umbo dogo sio Nzito,, naombeni mnipe mazuri yake na mabaya yake
Mazuri ya simu za kijapan
1. Ina esim, Muhimu siku hizi sababu mitandao yetu mingi inasuport, inasaidia Sana kama Una line ambazo huzitumii Sana.
2. Micro SD na 3.5MM jack ambazo simu nyingi za siku hizi hupati.
3. Ina usb 3.2, feature ambayo simu chache Sana inayo, unaweza Tumia simu kama desktop na monitor ama TV.
Hizi feature ni Universal kwa simu nyingi za kijapan.
Pia kwa specific hio simu perfomance sio mbaya, kioo kizuri etc.
Mambo ya kujua
-Igzo display haina spea, ukivunja kioo utaanza kuhangaika, nimeona vioo feki vya LCD vimeanza kuingia kwa simu za zamani Sina uhakika kama sense 8 nayo utapata.
-processor yake ni ya kizamani kidogo, battery kubwa ila ukaaji chaji utakua wa kawaida,
-itachaji Taratibu, pengine inafika masaa 2 mpaka kujaa.
-lte band hakuna 20 na 7 utapata Tu Tigo Mjini nje ya mji utakua limited na Voda na Airtel.
Overall ni simu nzuri kama unaipata kwa bei zetu hizi around 300K kushuka.