Shares za NMB, DCB na NICOL !

smak786110

Member
Jan 24, 2008
90
2
Please share your knowledge on the following regarding DSM Stock Exchange:-

1) Why is NMB shares taking so long to come out ? Are they doing some under table works with their Profit and Loss Account or something ?

2) Do you think its worth investing in DCB (DSM Community Bank) shares ?

3) What about NICOL SHARES ? Have you bought share in it ?

4) NIC sold shares privately few weeks ago, is that true ???
 
Please share your knowledge on the following regarding DSM Stock Exchange:-

1) Why is NMB shares taking so long to come out ? Are they doing some under table works with their Profit and Loss Account or something ?

2) Do you think its worth investing in DCB (DSM Community Bank) shares ?

3) What about NICOL SHARES ? Have you bought share in it ?

4) NIC sold shares privately few weeks ago, is that true ???


ni vizuri kabla ya kuamua kununua shares zozote upitie
financial reports zao. bahati mbaya sikuweza kuona
kwenye web site ya nmb sehemu inayozungumzia
masuala ya "investors" jambo ambalo
nadhani ni upungufu mkubwa. aidha sikufanikiwa kuona kama
dsm wana web site.

kabla hujanunua shares ni vyema ukajua kwa nini unanunua hizo shares
mfano jee ni kwa kunufaika haraka haraka (kwa kuamini shares zitapanda
bei hivi karibuni ili uziuze) au unania ya kuzishikilia kwa muda mrefu.

nakutakia mafanikio.
 
Suala la kununua shares zinazotolewa awali (Initial Public Offering-IPO) linapigiwa sana debe na watu wa finance.Wanasema siku zote bei za shares zinapotolewa kwanza huwa zinakuwa hazijafanyiwa valuation ya kujitosheleza kwahiyo bei inayotolewa katika IPOs huwa inakuwa mchekea (Underpriced) kwahiyo share hizo zikianza kuuzwa kwenye Secondary Market (Stock exchange) DSE kwa case ya Tanzania ambako brokers na potential investors wanafanya thorough analysis ya potentials za kampuni mara nyingi hutokea kwamba bei hupanda maradufu na maranyingi kwa uzoefu wa Tanzania hata kwa 30%.

Hii ina maana kama ulinunua share ambazo zilikuwa zinauzwa shilingi mia kwa kila share mara zinapoanza kuuzwa DSE inaweza kuuzwa hata kwa sh.130/=.hivyo kukupa faida ya shilingi 30/= kwa kila share ambayo katika hali ya kawaida ni faida kubwa kuliko hata inayotolewa katika T-bills kwamfano kwa mwaka.

Point nayotaka kusisitiza ni kwa wanunuzi kupitia prospectus ya makampuni husika na kuona kama faida na potential ya kukua kwa kampuni inakuvutia baada ya hapo unaweza kununua share kwa kampuni.NMB itakuwa sehemu bora zaidi ya kuwekeza kwa wale wanaoamini katika aina hii ya uwekezaji.
 
ni kweli watu hukimbilia ipos na kutokana na kukimbilia utakuta bei ya stock husika hupanda pasipo mpangilio. hata hivyo inafika wakati bei hiyo hukwama na kuanza kujiadjust na mara nyingi hurudi chini. hapo ndio upo umuhimu wa kujua kama umenunua kwa faida ya haraka haraka au wataka kuzishikilia shares zako.

bahati mbaya wengi wakinunua shares na kuona zimepanda bei kwa kasi zinapoanza kushuka hawaziuzi shares zao kwa matumaini kwamba zitapanda tena na matokeo yake ni hasara.

kama wewe ni mshiriki wa soko la pesa mdogo (mathalani uwezo wako ni kununua shares chache mfano 100 tu) ni bora ukawa makini na kungoja bei zijiadjust halafu uone kama hiyo kampuni inamatumaini ya kupanda siku za usoni.

kununua na kuuza inabidi ukumbuke kuna gharama za mabrokers kila ununuapo na kuuza. pia kuna kodi ya mapato kila ukiuza kwa faida.

bado naamini financial reports za miaka 3-5 zitasaidia sana katika kufanya maamuzi. prospectus sidhani kama ni njema, kumbuka prospectus ya tol.
 
Back
Top Bottom