SHANGiNGI APORA MUME WA MTU DAR!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SHANGiNGI APORA MUME WA MTU DAR!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Boflo, May 3, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Monday, May 03, 2010 10:09 AM
  KATIKA hali isiyo ya kawaida mtandao huu ulishuhudia mwanamke mmoja akilia kwa machungu baada ya kushuhudia mwanandoa wake akibebwa na moja ya mashangingi ya mtaa huo.
  Dada huyo alikadiria kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 26 aliangua kilio cha nguvu na kushindwa kujizuia baada ya kushuhudia mume wake kipenzi akiondoka na shangingi hilo.

  Tukio hilo la aina yake lilkitokea jana majira ya saa 11:45 jioni, katika maeneo ya Kinondoni Manyanya baada ya shangingi hilo kufika nyumbani kwa dada huyo na kuondoka na mume wake.

  Mtandao huu ulishuhudia tukio hilo na kukuta dada huyo akilia na watu kujaa mtaani baada ya kuangua kilio cha nguvu ambapo kilivutia watu wengi na kujaa eneo hilo.

  Mtandao huu ulijaribu kuwahoji watu wawili watatu ambao ni majirani na mwanamke huyo walidai kuwa alikuwa akilia kwa kuwa ameshuhudia mume wake akiondoka na shangingi moja maarufu mtaani hapo jambo ambalo amefanya aamini alilokuwa akiambiwa na majirani zake.

  “Ujue dada, huyu analia kwa machungu kwa kuwa mume wake ametekwa na shangingi moja la hapa mtaani ambalo kazi yake ni kuchukua waume za watu, na tulikuwa tunamueleza alikuwa hatuamini sasa leo kashuhuda mwenyewe’ ndio mana analia hivyo” walisema

  Ilidaiwa kuwa mume wa dada huyo ni kijana naye anayekadiriwa kuwa na miaka 28 hadi 30 alitekwa kimapenzi na mama huyo ambapo ilidaiwa alikuwa akimsaidia katika mambo mengi ya kimaisha na kumpa pesa na kijana huyo kunogewa na huyo mama anayekadiriwa kuwa na miaka 40 hadi 45.

  Ilidaiwa kuwa kijana huyo kabla ya kutekwa na jimama hilo alikuwa akijishughulisha na biashara ndogondogo akiuza viatu vya mitumba kupitisha mitaani.

  Alipoona amepiga hatua moja alikwenda kijijini kwao Iringa na kwenda kuoa na kurudi na mke wake huyo ambaye alishakuwa amezaa nae mtoto mmoja wa kiume ambaye ana umri wa miezi 11 sasa.

  Majirani hao walidai kuwa kijana huyo alianza kubadilika tabia na pia akibadilisha biashara na kufungua mabanda ya biashara sehemu mbalimbali ikiwemo kariakoo na kinondoni.

  Majirani waliposhtukia kuwa shangingi hilo maarufu ndilo linalomtunza kijana huyo walimtonya mkewe ambaye hakuamini na hakutaka kusikia stori hizo.

  Siku ya tukio jimama hilo alifika nyumbani kwa kijana huyo na gari yake aina ya Toyota RAV 4 na kupiga mlio ulioashiria yuko nje ya nyumba hiyo na kijana huyo alitoka nje na kupanda garini na kuondoka naye.
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhh labda ni business partner, tusidraw conculutions because of their genderz
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Boflo umebadili jina nini? kutoka lile la Bw.....
   
Loading...