shamrashamra arumeru-polisi wanakimbia wananchi

Tulianza na Mungu, Tumemaliza na Mungu, Asanteni saaana makamanda kwa kutupa raha!!!!
 
Sera za chadema nazipenda sana lkn kinaniboa zaidi ktk suala zima la ubinafsi udini na ukabila, wala hakuna ubishi chama hiki kitapoteza dira
 
Kila la kheri wandugu msherekee kwa amani,muwaonyeshe watu kuwa cdm si chama cha vurugu kama ambavyo huwa wanadai.hongera nassari.
 
Ni kweli kabisa mkuu, lazima tusherehekee ushindi wetu kwa njia za amani ili kuzidi kuwadhihirishia kina Lusinde na wenzake kwamba hiki chama makini - viongozi makini & wanachama makini!

Huu sasa ulimbukeni, hata sherehe mnataka kuzipangia kanuni? wenzenu walikoswa koswa kumwagiwa matindikali, kupigwa risasi, kukatwa mapanga na mashoka, macho yamewavimba kwa mabomu ya machozi waliyovurumishiwa na mapolisi ili kuwatisha waachane na mkakati wa kulinda kura! leo wameshashinda mnataka washerehekee kinyonge, lazima, narudia lazima washerehekee kwa kujinafasi, POLICE MUST STAY AWAY TO SPARE OUR ANGER WHILE CELEBRATING. THEIR PRESENCE IS MOKING. Inatukumbusha matusi ya lusinde.
 
Back
Top Bottom