Shambulizi moja la bomu nchini Uturuki limewaua wanajeshi 13

Kazetela

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,547
2,000
Shambulizi moja la bomu nchini Uturuki limewaua
wanajeshi 13 waliokuwa ndani ya basi na
kuwajeruhi wengine 48.
1481976981193.jpg

Mlipuko huo uliharibu basi hilo ambalo lilikuwa na
wanajeshi waliokuwa wameruhusiwa kusafiri kwenda
soko moja, mwa mujibu wa msemaji wa jeshi.

Picha kutoka eneo ambapo mlipuko huo ulitokea
zilionysha basi hio likiwa limeharibiwa kabisa na
shimo kubwa likionekana upande mmoja.

Shambulizi la Uturuki limefanywa na kijana wa
miaka 14
Uturuki:Kundi la IS linapaswa kutokomezwa
Mlipuko huo unatokea wiki moja baada watu 44
kuuawa na shambulizi la bomu mjini Istanbul,
lililodaiwa kufanywa na wanamgambo wa kurdi.

Uturuki imekumbwa na misurusu ya mashambulizi
mabaya mwaka huu wa 2016 mikononi mwa
wanamgambo wa kurdi.

Baibu waziri mkuu Veysi Kaynak alisema kuwa
shambulizi hilo lilikuwa sawa na lililoendeshwa na
wanamgambo mjini Istanbul.

Serikali imeweka marufuku ya muda ya
kutotangazwa kwa shambulizi hilo.
Seriklia imewka mmarufuku a uda ya kutangazwa
kjwa shmbualia hilo.
 

Fyangu fyosa

Senior Member
May 6, 2016
132
250
kwa nni serekali ya uturuki ilivunja makubaliano ya amani na wakurd, maana baadhi ya haya yasingetokea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom