Shamba lenye rutuba halihitaji mbolea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shamba lenye rutuba halihitaji mbolea

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzizi wa Mbuyu, Jun 1, 2009.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ni kweli jamani mbolea ipelekwe kwenye mashamba yasiyokuwa na rutuba ili nayo pia yaweze 'kutoa mazao bora'.

  Utakuta mtu anauwezo mkubwa kifedha anaoa au anaolewa na mtu mwenye uwezo pia, kwanini watu wenye uwezo wasioe au kuolewa na watu wasiokuwa na uwezo ili angalao tupunguze umasikini katika jamii zetu?
  Angalia mifano;
  Mume mbunge mke mbunge
  Mume spika mama waziri
  Mama ana degree tatu mme anazo tatu
  N.k...
  Tena wako warembo wa nguvu ila hawajasoma kabisa ila wako safi tu na maadili yao yako juu! Pia mijibaba iliyo kwenda angani lakini iko hoi kimaisha!

  Jamani mnionaje hii....ni sawa kuliongezea mbolea shamba lenye rutuba?
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  birds of a feather flock together....unaijua hiyo?
  watu wa asili moja, hukaa pamoja. Sasa mimi nina degree kweli ntaendana na mtu asiye na degree? Hakuna kitu kama kupenda ghafla tu 'spontaneously falling in love'. Wewe unayemchagua unakuwa umeshamchuja bila kujua (unconsciously) kwa kutumia vigezo vingi ulivyowekewa kutokana na mazingira uliyoishi. Haya yote yanatokea ndani kwa ndani bila wewe kufikiria.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu ume simplify sana.Nikuulize maswali machache:
  Mazingira ya kukutana wapendanao, kitu cha kuwavuta pamoja je?
  Kwani hao uliowaorodhesha walikuwa hivyo toka wanakutana?
  Kupendana hakuangalii vigezo unavyotaka wewe - kuna wenye kupendana kwa sababu, kuna wale wanaopendana kwa sababu wanapendana n.k.Hakuna kanuni maalum.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu mambo ya mapenzi si lazima yahusiane na mapene ndugu.....Love is someting natural while money is just artificial thing!
   
 5. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Inategemea mlikutana kwenye mazingira gani na asili ya mtu.
  Lakini kuna wanaume wengi wasomi na wenye uwezo wameoa wasichana wasiosoma na wasiokuwa na chochote anapoanza kukaa naye ndo anamuendeleza,
  elimu ni kigezo, lakini sidhani kama ni kigezo muhimu sana wakati wa kuchagua mke au mume, kuna watu hawajasoma wana biashara zao nzuri wanazimanage na wana akili zingine za maisha na wametulia. inategea mtu unataka nini, kama huna majivuno au sifa ( nachukia wanaume wenye sifa sana) au kutaka watu wakuone
  Na wanaume wabinafsi anaona akioa mtoto wa maskini atamtegea kwa kila kitu na yeye ana umimi anataka kila kitu chake kiwe chake mwenyewe badala afikirie nitamuendelezaje na yeye aweze kusimama kwa miguu yake.
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Niliogopa ningeingia sana ningekuwa sijaacha nafasi kwa wachangiaji, kuhusu kuwa hivyo tangu wanakutana, siyo woote ila mtu Kama John Malechela alikuwa tayari kigogo alipokutana na Anne Kilango. Hapa nilikuwa nazungumzia new looove! tuache kutafuta wenzi wenye uwezo tuuu!
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Wewe "mkali" sana sister nimekukubali, ila hii kauli imenisisimua kweli!! na nadhani sijaelewa kwanini uwachukie kiasi hicho, ndivyo walivyo tu dada!
   
 8. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sikiliza nikuambie kaka yangu, mwanaume mwenye sifa na majivuno ni lazima atakudharau tu hata iweje. hata ukifanya zuri au ukijitahidi sababu yeye ameshazoe kujiupgrade anakuona wewe siyo kitu kabisa, kazi ni kukuvunja moyo.halafu mwanaume mwenye sifa hajifichi siku ya kwanza tu utajua.
   
 9. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Haya bwana, una haki ya kuamini hivyo. Ila usisahao watu wengine wanapenda sana kujikweza lakini ni watu wastaarabu kabisa kwenye mahusiano. ........ ila nadhani kweli kuna hoja hapa, nimekumbuka.., nina jamaa yangu mmoja wa Iringa yule bwana anapenda kujisifu yaani Jose Morinyo cha mtoto!! Lakini huwa anamjibu mkewe kunya mno!, yaani hata mbele za watu!!
   
Loading...