Shaka: Vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA viwe huru kususia uchaguzi

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Habari za leo wadau.

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake Wa Uenezi komledi Shaka kimesema Vyama vya upinzani viwe huru kabisa Kususia uchaguzi hususani CHADEMA ambao ndio wamekuwa wakisema watasusia chaguzi zozote bila Tume huru na Katiba Mpya.

Shaka amesema wakisusa CCM wao wataendelea kula.

Wanachadema pokeeni dongo Hilo mtaamua kula au kushinda na njaa.👇

=====

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamidu Shaka amevitaka baadhi ya vyama vya upinzani kuwa huru kususia uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ni haki yao na hata vikifika maamuzi hayo chama hicho hakitayumba kwa kuwa kimejipanga kuchukua tena dola mwaka 2025.

Ameyasema hayo Unguja wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo amesema kuwa mapokezi makubwa aliyoyapata Rais Dkt. Mwinyi ni ishara ya wazi kuwa wananchi wameridhishwa na uongozi wake.

“Nimekuwa nikisikiasikia wameanza kusemasema kwamba wanafikiria sijui tutasusa, sasa sijui msuse msisuse shughuli ipo kitu hiki hapa. Niwaombe wana-CCM wenzangu msipoteze muda wa malumbano na majibizano, tuna kazi ya kujenga chama, tuna kazi ya kujenga nchi hii,” amesema.

Ameongeza kuwa kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama hicho ni ‘kutesti mitambo’ tu na kwamba muda ukifika wapinzani wataupata ujumbe, hivyo wakae kwa kutulia kwa kuwa hakuna mjadala katika hilo na wala hakuna kubembelezana.

CHANZO: Swahili Times
 
Habari za leo wadau.

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake Wa Uenezi komledi Shaka kimesema Vyama vya upinzani viwe huru kabisa Kususia uchaguzi hususani CHADEMA ambao ndio wamekuwa wakisema watasusia chaguzi zozote bila Tume huru na Katiba Mpya.

Shaka amesema wakisusa CCM wao wataendelea kula.

Wanachadema pokeeni dongo Hilo mtaamua kula au kushinda na njaa.👇View attachment 2444592
Japo naunga mkono hoja, ya "ukisusa sie twala...," na siungi mkono hii tabia ya kususa susa.... Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto? na hapa Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! na Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA is almost dead, due to deadly mistakes! This is your only survival -- do or die. Msirudie kosa

Lakini kama wanasusa for genuine reasons za kutotendewa haki, kama tulivyo shauri hapa Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Najua by now wasoma trends wanajua the consequences za kutotenda haki kwenye uchaguzi, sisi washauri huru tuliisha shauri kabla Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! hivyo Shaka asijitape wakisusa kwa kutetendewa haki sisi twala, badala ya kula wakajikuta wao ndio wanaliwa vichwa!.

Karma haina mswalie Mtume, walishindwa kumlinda Blaza, karma ikafanya yake!, ili kumlinda Maza na karmic consequences, sisi tunao ijua karma, lazima tumsaidie Maza kwa kumweleza ukweli ili aepuke the consequences na yeye asije... hivyo kwa kuanzia tumemshauri Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
 
Habari za leo wadau.

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake Wa Uenezi komledi Shaka kimesema Vyama vya upinzani viwe huru kabisa Kususia uchaguzi hususani CHADEMA ambao ndio wamekuwa wakisema watasusia chaguzi zozote bila Tume huru na Katiba Mpya.

Shaka amesema wakisusa CCM wao wataendelea kula.

Wanachadema pokeeni dongo Hilo mtaamua kula au kushinda na njaa.👇View attachment 2444592
Nikimuonaga huyu Shaka na yale mambo yake kiasi cha kufikia kuvunja familia za watu leo yupo ngazi za juu sana huko CCM akiwaacha kwa mbali wacha Mungu, watu smart na wenye akili zao huwa inanipa fikara zaidi juu ya fumbo la maisha.
 
Jikite kwenye hoja achana na maisha binafsi ya mtu.
 
Ni kweli alichosema huyo jamaa, mbinu ya kususa haiwezi kuwa na nguvu sana kwasababu CCM itawaambia vyama rafiki vyao vya upinzani washiriki, nao watashiriki huku wakisema uchaguzi ulikuwa huru na haki, na wakija waangalizi wa kimataifa nao waseme hivyo, na shughuli ndio iishie hapo.

Kwani binafsi naamini, bila kufanyika jitihada za ziada, naona haya madai ya Katiba Mpya, na Tume Huru ya uchaguzi, yatakuwa endelevu yasiyojulikana lini utakuwa mwisho wake, hivyo kuendelea kuinufaisha CCM.

Muhimu Chadema wasionekane wanahodhi madai ya Katiba Mpya, kwani hii inawapa CCM sababu nyepesi za kujibu hoja hiyo ikiwemo wananchi hawali Katiba Mpya.

Naona kuna haja sasa kwa Chadema kuhakikisha wanapeleka somo la umuhimu wa Katiba Mpya kwa makundi mengine ya kijamii, ikiwemo, kilimo, uvuvi, wafanyabiashara, na kada nyingine.

Ili hawa wakishapewa somo na kulielewa, nao wageuke walimu, waanze kupaza sauti zao kwa pamoja, kwa kufanya hivyo; kwanza itasaidia kuondoa dhana kwamba madai ya Katiba Mpya ni ya Chadema, au ya kisiasa, lakini pia, itayafanya madai ya Katiba Mpya yachukuliwe kwa uzito zaidi, na kuleta impact kubwa zaidi ya ilivyo sasa, hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kufikia malengo kwa wakati.
 
Ni kweli alichosema huyo jamaa, mbinu ya kususa haiwezi kuwa na nguvu sana kwasababu CCM itawaambia vyama rafiki vyao vya upinzani washiriki, nao watashiriki huku wakisema ulikuwa huru na haki, na wakija waangalizi wa kimataifa nao waseme hivyo, na shughuli ndio iishie hapo.

Bila kufanyika jitihada za ziada, naona haya madai ya Katiba Mpya, na Tume Huru ya uchaguzi yatakuwa endelevu yasiyojulikana lini utakuwa mwisho wake, hivyo kuendelea kuinufaisha CCM.

Naona kuna haja sasa kwa Chadema kuhakikisha wanapeleka somo la umuhimu wa Katiba Mpya kwa makundi mengine ya jamii ikiwemo kilimo, uvuvi, wafanyabiashara na kada nyingine.

Ili hawa wakishapewa somo na kulielewa, nao wageuke walimu, waanze kupaza sauti zao kwa pamoja, kwa kufanya hivyo kwanza itasaidia kuondoa dhana kwamba madai ya Katiba Mpya ni ya Chadema, au ya kisiasa, lakini pia, itayafanya madai ya Katiba Mpya yachukuliwe kwa uzito zaidi, na kuleta impact kubwa zaidi ya ilivyo sasa hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kufikia malengo kwa wakati.
Lakini hao wananchi si ndio wenyewe waliyotaka hiyo katiba mpya sasa inakuaje tena waone katiba mpya ni hitaji la wanasiasa?
 
Kutokana na Duru za kuaminika humu JAMVINI!

2025 ni mbali Sana,yaani inawezekana tukawa na katibu mwenezi wa chama mpya na Mwenyekiti pia!!

Mwambieni shaka atafakari maneno ya mzee makamba! HALAFU ajiulize Kati ya aliemweka hapo na Huyo mzee nani ananguvu kwenye chama!

Pia"Hakika Allah yu pamoja na wenye subrah"!

Mwambieni Tatizo la ccm siyo Chadema Bali "MABADILIKO YALIYOKUSUDIWA NA DOLA KWA MSTAKABALI WA TANZANIA MPYA YA KATIBA MPYA"

Pia amwambie Mwenyekiti aondoe hicho KINYAGO cha "Kikosi kazi cha Mkandala ambacho kinamdanganya kwamba kinabagaza maagizo ya DOLA KUHUSU Katiba MPYA"

Hicho kikosi cha mchongo ni kirusi kinachotafuna mifupa ya uongozi wake!!

Mwambieni amwambie Mwenyekiti a "GO FOR IT" yaani aikumbatie katiba mpya kama mpenzi wake mpya wa mwanzoni KABISA wa MAKUZI yake na sio kuhepa kimchongo kama hivi SASA!!

Pia Mwenyekiti ajiulize "MAISHA YANATAKA NINI ZAIDI!!?KAMA KAZI UMEPATA,WATOTO WAMESOMA NA WANA KAZI,YANATAKA NINI ZAIDI!!?

"USHAURI HURU KUTOKA KWA MWANACCM MWENYE AKILI TIMAMU AMBAYE HAJALEWA MADARAKA NA KUSAHAU ASILI YA KIAPO "NITASEMA KWELI DAIMA,UONGO KWANGU MWIKO""!
 
Lakini hao wananchi si ndio wenyewe waliyotaka hiyo katiba mpya sasa inakuaje tena waone katiba mpya ni hitaji la wanasiasa?
Kinachofanya ionekane Katiba Mpya ni hitaji la kisiasa ni kutokana na mpiga debe mkuu kuwa chama cha siasa, hii ndio sababu inayotumiwa na CCM kuwafunga midomo wapinzani wao kuhusu hayo madai.

Lakini kama madai hayo yangetokea kwenye makundi tofauti ya kijamii, naamini CCM wangekuwa kwenye wakati mgumu zaidi ya ilivyo sasa, na kujikuta wanalazimika kuyafanyia kazi.

Hii mbinu ya kuunganisha makundi tofauti japo itaonekana itachukua muda mrefu, lakini naamini kama ikiwezekana, ndio itakuja na mafanikio makubwa zaidi ya ilivyo sasa.
 
Nikimuonaga huyu Shaka na yale mambo yake kiasi cha kufikia kuvunja familia za watu leo yupo ngazi za juu sana huko CCM akiwaacha kwa mbali wacha Mungu, watu smart na wenye akili zao huwa inanipa fikara zaidi juu ya fumbo la maisha.
Mchicha mwiba?
 
Back
Top Bottom