Shaka Hamdu Shaka amelala nyumbani kwa Balozi Ndugu Iddi Mwaibaje

budget

Member
Feb 23, 2015
42
27
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka amelala nyumbani kwa Balozi Ndugu Iddi Mwaibaje mwenyekiti wa shina namba 1 Kata ya Chapwa Jimbo la Tunduma. Asubuhi ya leo amejumuika na uongozi na wanachama wa shina hilo kupata chai pamoja.

Akiwa katika shina hilo Ndugu Shaka aliushukuru uongozi na wanachama wa shina kwa ukarimu na kuwataka viongozi wengine wa chama na serikali kuwa na utamaduni wa kupenda kukaa na kula pamoja na wenyeviti wa mashina kwani inawapa ari zaidi katika majukumu yao na kujenga mshikamano kati yao. Pia aliwasilisha salaam za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo kwa wanachama wa shina hilo.

Alieleza madhumuni ya ziara yao ni kuendelea kuimarisha uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025. Aidha pamoja na madhumuni hayo wanasikiliza na kupokea kero za wananchi kwa ajili ya kusukuma utatuzi wake.

Amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa halmashauri ya mji Tunduma kwa kuiamini CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kuwachagua madiwani wote, Mbunge na Rais kwa ushindi wa kishindo.

"Imani yenu kwa CCM tutailinda, tutaitunza na tutaipa thamani kwa kuwaletea maendeleo ya kweli na kuimarisha huduma kwenu. Endeleeni kutuunga mkono na kumuunga mkono Mhe Rais Samia na serikali anayoiongoza." Alisema Shaka.

Alimpongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Tunduma, madiwani na wataalam wake kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ambapo aliwasisitiza ongezeko la makusanyo likaonekane kwa wananchi kwa kuimarisha huduma na kuwajengea mazingira mazuri ya kiuchumi ili washiriki vizuri katika kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.​

IMG-20210710-WA0058.jpg
IMG-20210710-WA0056.jpg
IMG-20210710-WA0054.jpg
 
Huko nikuwadhalilisha mabalozi,
Angelala kwa balozi mwenye nyumba ya nyasi na maji hakuna.
Posho alizopewa za malazi amerudisha ofisini.

Huo upendo wakinafiki.mabalozi wa mjini mbona ni watumishi wastafu wako vizuri
 
Naona kaamua kwenda from grassroot..
Sisi wapinzani tuko twitter..
 
Akili zake sawa na za mama tu , wote hamna kitu, sasa hiyo ndio inamsaidia nini mwananchi, wana fanya cheap propaganda. Mama anaendelea kuupiga mwingi sana.
 
Nilifikiri amepelekwa na balozi kuchota maji kwenye mito vijijini huko aone adha
 
Akili zake sawa na za mama tu , wote hamna kitu, sasa hiyo ndio inamsaidia nini mwananchi, wana fanya cheap propaganda. Mama anaendelea kuupiga mwingi sana.
Sio cheap propagana,,anaimarisha chama anzia ngazi za chini,,inaitwa winning heart and mind,,
Hao wanashina hiyo ziara itabaki mioyoni na vichwani mwao,siku ya uchaguzi kura kedekede,,🤗🤗
 
Ni hapo Tunduma ambapo watu wanakunywa mafuta upande wa pili

Yeye anakunywa chai na balozi
Anafufua uchumi au anajaza tumbo lake
 
Vijana mnakosa hoja za kujenga..........hii nayo ni hoja ya kuleta hapa. Njaaaaaaaaaaa ni taabu kwa kweli
 
Back
Top Bottom