Kwani Askari waliozuia watu wasiingie kwenye ukumbi wa mahakama walikuwa chini ya utawala wa Chama gani, na chini ya Rais gani?
Na kama CCM ni chama kinachofuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, Shaka atuambie Askari waliozuia watu kuingia ukumbini walitumia sheria gani kufanya hivyo, na kama walitumia sheria kwa nini maamzi yao yalitenguliwa na mahakama?
Na kama jeshi la Polisi halikufuata sheria je Shaka haoni aibu kuzungumzia demokrasia ambayo haipo ndani ya jeshi, na mahakama ilitoa uamzi baada ya watu kulalamika?
Shaka atuambie ikiwa mahakama ilitenda haki kuwaruhusu watu kuingia kwenye ukumbi wa mahakama, ni hatua gani ya Chama na serikali yake inawachukulia hao polisi waliovunja sheria?
Vinginevyo shaka tutamtilia shaka kwa uwezo wake wa kufikiri.