shairi


Mandesy

Mandesy

Member
Joined
Mar 22, 2018
Messages
89
Points
125
Mandesy

Mandesy

Member
Joined Mar 22, 2018
89 125
Malenga napiga hodi, mlango muufungue,

Mimi muhenga wa jadi, ngoja niwaelezee,

Kuhusu huyu hasidi, mshamba wa kipekee,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani.Tumeyafuga majoka, sasa yanatutafuna,

Misumu inawayatoka, hakuna atayepona,

Twabaki kuweweseka, Majoka yameungana,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani.Nyoka anapenda sifa, utadhani ni mhaya,

Alipopewa taifa, akaanza roho mbaya,

Amegeuka maafa, twamkumbuka Jakaya,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamaniAmejivika umungu, ili watu wamuabudu,

Anawaponda wazungu, kumbe anayo madudu,

Kajiweka kwenye mbingu, anatuona vibudu,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamaniKajijazia wapambe, wale walamba miguu,

Wengi wao wanywa pombe, wanaupenda ukuu,

Hata wale wala sembe, siku hizi wako juu

Watanzania wa leo, sio wale wa zamaniKitu cha kwanza mshamba, hana ujanja wowote,

Kila kucha kujigamba, wakati ni kiokote,

Wapambe wanampamba, ili chakula wapate

Watanzania wa leo, sio wale wa zamaniAnaipenda misifa, aonekane mahiri,

Anadhani hatakufa, katika hii sayari,

Huyu mzee ni lofa, tena ni mtu hatari,

Watanzania wa leo sio wale wa zamani.Leo naishia hapa, kesho nitarudi tena,

Kidogo nimemchapa, kuiondoa laana,

Ameletwa na Nkapa, kumbe hana cha maana,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamaniMwisho
 
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
3,893
Points
2,000
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
3,893 2,000
Ndio maana walimu wa vivumishi na vina na mizani ya mashairi hamuajiriwi

Yaan mnavijimaneno vya udhaifu dhaifu fulani hivi
 

Forum statistics

Threads 1,285,664
Members 494,728
Posts 30,869,649
Top