Shairi: Watanzania wa leo

Mandesy

Senior Member
Mar 22, 2018
115
125
Malenga napiga hodi, mlango muufungue,

Mimi muhenga wa jadi, ngoja niwaelezee,

Kuhusu huyu hasidi, mshamba wa kipekee,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani.



Tumeyafuga majoka, sasa yanatutafuna,

Misumu inawayatoka, hakuna atayepona,

Twabaki kuweweseka, Majoka yameungana,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani.



Nyoka anapenda sifa, utadhani ni mhaya,

Alipopewa taifa, akaanza roho mbaya,

Amegeuka maafa, twamkumbuka Jakaya,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani



Amejivika umungu, ili watu wamuabudu,

Anawaponda wazungu, kumbe anayo madudu,

Kajiweka kwenye mbingu, anatuona vibudu,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani



Kajijazia wapambe, wale walamba miguu,

Wengi wao wanywa pombe, wanaupenda ukuu,

Hata wale wala sembe, siku hizi wako juu

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani



Kitu cha kwanza mshamba, hana ujanja wowote,

Kila kucha kujigamba, wakati ni kiokote,

Wapambe wanampamba, ili chakula wapate

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani



Anaipenda misifa, aonekane mahiri,

Anadhani hatakufa, katika hii sayari,

Huyu mzee ni lofa, tena ni mtu hatari,

Watanzania wa leo sio wale wa zamani.



Leo naishia hapa, kesho nitarudi tena,

Kidogo nimemchapa, kuiondoa laana,

Ameletwa na Nkapa, kumbe hana cha maana,

Watanzania wa leo, sio wale wa zamani



Mwisho
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom