Shairi : Pendo ni kitu adhimu

yussuf hajj

Member
Jul 22, 2015
8
2
Pendo ni kitu adhimu ,Mungu ametuumbia
Tupendane binadamu ,Ushenzi kuukimbia
Tusiwe wana haramu ,Wenzetu kuwaibia
Pendo kitu cha thamani , tena kitu cha furaha.



Raha ya pendo kupendwa , Na yule umpendae
Usitamani kutendwa , utatamani ujiue
Uhai kuuondowa , Akhera uadhibiwe
Pendo kitu cha thamani , Tena kitu cha furaha
 
Pendo ni kitu adhimu ,Mungu ametuumbia
Tupendane binadamu ,Ushenzi kuukimbia
Tusiwe wana haramu ,Wenzetu kuwaibia
Pendo kitu cha thamani , tena kitu cha furaha.

Raha ya pendo kupendwa , Na yule umpendae
Usitamani kutendwa , utatamani ujiue
Uhai kuuondowa , Akhera uadhibiwe
Pendo kitu cha thamani , Tena kitu cha furaha
Yusufu Haji jamani, naiunga hoja yako,
Pendo kitu cha thamani, ndani ya nafisi yako,
Tangu enzi za zamani, ni mambo ya roho yako,
Pendo kitu cha thamani, na ndio furaha
yako,
Paskali
 
Paskali mayalla , hakika ni mzalendo

Usiejua kulala, kuuhimiza upendo

Usietaka chakula , kilicho vingi vishindo

Udumishae furaha , na kufata nzuri nyendo.
 
Back
Top Bottom