Shairi: Nyama Ya Bundi

Shairi: Nyama Ya Bundi

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
NYAMA YA BUNDI.

1)ni tamu kama halua,ila ni chungu kuila.
Kumeza hutoamua,kama ukila kwa hila.
Mpishi wajipikia,pishi liso na fadhila.
Nyama ya bundi si tamu,vipi unatuwindia.

2)nyumbani anapotua,chumvi moto twaichoma
Ili apate kimbia,yu wako ka jiduma.
Mbona tena amkia,jasho lake linachoma.
Nyama ya bundi si tamu,vipi unatuwindia.

3)panzi unawazuia,wasije.kula mpunga.
Tadhani tamalizia,sidhani wao ni wanga.
Tazani aliwachia,jozani unawazinga
Nyama ya bundi si tamu,vipi unatuwindia.

4)pilipili waringia,si wewe uloipika.
Bundi watukaangia,hadi kwako italika.
Wanao wawapakia,wawenzako wawacheka.
Nyama ya bundi si tamu,vipi unatupikia.

5)mzimu ukitokea,bundi atakurishia.
Jiko litapopotea,manyoya takurushia
Sikio halitosia,kucha tutafungishia.
Nyama ya bundi si tamu,vipi unatuwindia.

Shairi=NYAMA YA BUNDI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
 
Aisifuye mvua, hakika imemnyea,
Imetoteshwa pua, kama mbegu kimea,
Unaanza kwa kupakua, tafuna maji mezea,
Kama kichungu huonjwa! Mwenzetu we kigagula!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom