Sayansi ya mapepo.


Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,655
Points
2,000
Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
2,655 2,000
SAYANSI YA MAPEPO.

Maharage maharage,maharage leo kala
Sharubati kawa mbege,kelele kila mahala
Twiga kaota matege,na kijipembe cha swala
Hayakua ni matusi,pale akemea pepo.

Kweli mlichokiona,ile siyo sura yake
Yule ni kakakuona,ajilia vilo vyake
Vipi nyama ilo nona,fisi aipige teke
Alikwapua mfupa,leo watoka puani.

Alizifanya riwaya,akalala na bunduki
Akamsuta wa kaya,nusu angetoka nduki
Chai ikaitwa shaya,kwa nguruwe ni mkuki
Kweli simu simu janja,wajanja yawaumbua.

Chozi la madhabahuni,nalikumbuka shairi
Nilomuhisi muhuni,leo kavaa Hariri
Akitua kanisani,si mchawi ni sihiri
Ukitoa misukule,si upako ni uganga.


Katu hawatoamini,waliolishwa matango
Yenye miba ya porini,wameshageuzwa bango
Vipi uwe muumini,na ukushinde mpingo
Kumbe kichaa cha mbwa,humpata hata simba.

Hata wale wafutuhi,wazee wa kuchekesha
Leo ninawasabahi,mtaucheza mkesha
Ikifika hasubuhi,mvua itanyeesha
Mimi natulia tuli,baba na mwanae wale.

SHAIRI-SAYANSI YA MAPEPO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Forum statistics

Threads 1,296,485
Members 498,655
Posts 31,249,859
Top