Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,856
NIPE MOYO WAKO.
1)nahisi nilichelewa,kuwa nawe ewe wangu.
Moyo ulipolemewa,uliutoa machungu.
Mrembo ulinelewa,tukacheza lingulingu.
Basi nipe moyo wako,nami nikupe wa kwangu.
2)tena nifungie ndani,moyoni usinitoe.
Nikaangie maini,wenzangu niwatambie.
Niwe nawe barazani,furaha nijisikie.
Basi nipe moyo wako,nami nikupe wa kwangu.
3)vya nje hadi vya ndani,mpenzi unigaie
Unifutie huzuni,furaha nijisikie.
Na vitamu vya jikoni,mpenzi nikaangie.
Basi nipe moyo wako,nami nikupe wa kwangu.
4)unitengee mezani,halua mi nijilie
Usiniache gizani,na mwanga nimulikie.
Sitokwacha maishani,huzuni ujisikie
Basi nipe moyo wako,nami nikupe wa kwangu.
5)na mazao ya shambani,pamoja tujilimie.
Furaha ije nyumbani,watoto tufurahie.
Bilawe haki ya nani,ni bora niikimbie.
Basi nipe moyo wako,nami nikupe wa kwangu.
Shairi=NIPE MOYO WAKO.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
>>>>>kidogo tupige na mashairi ya mapenzi>>>>>>