Shairi: Nimeachiwa machela... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shairi: Nimeachiwa machela...

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Sungurampole, May 28, 2011.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu liko shairi moja niliwahi kusimuliwa zamani. Kwa bahati mbaya aliyekuwa anasimulia alikuwa mlevi mmoja na pia mimi nilikuwa mdogo sasa sikumuuliza jina la shairi wala mtunzi wake lakini atakuwa moja wa malenga wa siku nyingi.. Ninachkumbuka ni ujumbe wa shairi lile kuwa walikuwepo wavuvi wakivua wakaona watu wamebeba maiti na kama ilivyojadi ya waafrika nao wakajiunga ili kusaidiana kubeba baada ya kwenda muda wakibadilishana mara wakajikuta wako peke yao wavuvi na hawajui maiti ni ya nani, kafa na nini na wala anenda kuzikwa wapi? ..

  Nimejitahidi kulitafuta sehemu nyingi lakini sijafanikiwa kulipata

  naomba msaada wa yoyote anayelikukbuka - jina rasmi na/au mtunzi
   
 2. M

  Mwanangu Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sungurampole

  Na mimi niliwahi kusimuliwa ila nimesahau jina na mtunzi lakini nakumbuka jibu la kitendawili chenyewe. Nitajaribu kuulizia zaidi. Ni muda mrefu sijafuatilia habari za washairi lakini nadhani kina Koja Kuu, Sauti ya Kiza, Udogo si Hoja, Yoba kama bado wapo wanaweza kutusaidia.

  Mwanangu
   
 3. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,796
  Likes Received: 1,044
  Trophy Points: 280
  malenga wetu rtd na khalid ponera
   
 4. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ndumbayeye, mwnangu na maelenga shukhrani vipi tunaweza kupata beti zake? - mimi lilinikonga moyo sana nilipokuja tafakari nikiwa mtu mzima
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana jamvi MPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO?
  Mbona mmetuachia Machela?
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakika hizo ni tungo za zamani sana na shairi hilo la nimeachiwa machela mimi na rafiki yangu lilitungwa na mshairi maarufu sana kutoka Ikwiriri Rufiji kwa jina ni al marhum SHAABAN MUSA MKADARU. Ni lilitoka katika gazeti la ngurumo la taarih 26 April 1968 na kisa hicho ndio kisa kilichochukua muda mrefu sana katika magazeti ya tanganyika na kilifungwa mwaka 1975.

  Waliojitahidi kumpa majibu walikuwa pamoja na Sihiana Swalehe (madevu) wa Buguruni sokoni, Mzee Khalidi mtipa (ngondanee) wa Kibiti refiji, Shaaban Robert wa tanga, Saidi m Nyoka wa Tandika tambuka reli, Juma Maganga (Joka kuu) kutoka tabora, Saidi Sudi Andanenga (sauti ya kiza) wa kinondoni shamba na wengine.

  Nataliweka jamvini mara nikinafasika inshallah
   
 7. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Mkulu Br,
  ukiliiweka weka na majibu aliyopewa na Hasa ya SHABAAN ROBERT na SAUTI YA KIZA tafadhali
   
 8. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wakuu wangu nashukuru sana kwa majibu nasubiri kwa hamu nilipate kwa ukamilifu wake..juhudi zangu za siku nyingi zitakuwa zimezaa matunda
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika namelitafuta hapa katika maktaba yangu lakini silioni ila nimeagiza ahali zangu waliangalie huko Zanzibar kwenye mktaba yangu pia na nikilipata nitaliweka hadharani inshallah.

  Ngojeni nikupe Beti chache ninanzoweza kuzikumbuka


  1.Moja mbili tatu nne, namba tano siiioni,
  Bwana mtengenezaji, nakuomba samahani,
  Nipe kiliba cha maji, kinipooze kooni,
  Tumeachiwa machela mimi na rafiki yangu.

  2.Kwetu kumetungwa mila, tuseme au sheria,
  Ukiyaona machela, Ni wajibu kupokea,
  Huku ukijilamala, Na watu kusaidia,
  Tumeachiwa machela, mimi na rafiki yangu
  .
  ...
  .
  .
  .
  .
  .
  .Si mgonjwa wakusema, Na wala si wa kupumua,
  Kumbe yule ni maiti, Wenzetu wametuachia,
  ......
  Tumeachiwa machela mimi na Hasani wangu.


  Hizo ni baadhi tu (beti ya kwanza, pili na nyingine ambazo Marhum Shaaban Mussa Mkadaru wa Ikwiriri Rufiji alitunga.

  Nitawaletea inshallah mara nitakapo zipata.

  Dr Hamza Yousuf Al Naamaniy(Barubaru)
  154/ martaj ,Umm Hays ,
  Doha, Qatar
   
 10. C

  Choveki JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ahsante Barubaru,

  Umenikumbusha mbali na kunikumbusha kisa mimi kuwa mpenzi sana wa mashairi kwani watunzi hawa walikuwa wajuzi kwelikweli. Naona umetaja baadhi ya magwiji walomjibu, Je ulibatika kukutana au kufahamu baadhi ya hao magwiji?, Unajuwa nimekuwa najiuliza kutokana na mkabala wa dhiki na kubadika kwa mfumo wa kuwasilisha mashairi magazetini nahisi kama watunzi bora wengi ama wameamua kukaa kimya, au hawatumii vyombo vya habari kutoa tungo zao kama zamani. Pia vipindi kama mbinu za kiswahili, mashairi yetu nk vilikutanisha wengi kirahisi sana.
   
 11. Mbavu mbili

  Mbavu mbili JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 803
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  <br />
  <br />

  hongera sana kwa kumbukumbu nzuri ulizotupatia wengi wao hatukuwepo katika zama hizo kwani umri ulikuwa hauturuhusu...

  Asante kwa muadhama, barubaru ninakupa
  Kwa kazi iliyo njema, na kumbukumbu kutupa
  Utatukuka daima,ni heshima ninazokupa
  Aliyeachwa machela,katupa kisa kizuri
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakika mimi ni mmoja wa wapenzi wakubwa sana wa mashairi tokea nasoma darsa la tisa(form1) nilianza kutunga mashairi na hao niliokutajia wote nawajua.

  Na Huyo Marhum Shaaban Mussa Mkadaru nimefika mpaka kumzika kwao huko Ikwiriri km takriban 200 kutokea dar es Salaam njia kuelekea Mtwara.

  Nimezika akina Said Nyoka wa tambuka reli na wengine ninawasiliana nao mpaka leo. Kwani mie ni mmoja wa walezi wa chama cha washairi Tanzania.

  Nitaliweka hilo shairi pindi nikilipata.
   
Loading...