Shairi; Mtoto wa baba haguswi

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,205
4,403
MTOTO WA BABA HAGUSWI.

1)Shikamo kaka mkubwa,pole kwa kuchapwa fimbo.
Usihofu ndo ukubwa,umeepuka mkumbo.
Usiuwaze ubwabwa,ulochanganywa na shombo.
Huyo mtoto wa baba,haguswi eti haramu.

2)kweli kusema ukweli,nayo sasa ni matusi.
Ulikuwa ni dalali,leo una wasi wasi.
Pu kakupiga kabali,ngum nzito ya utosi.
Huyo mtoto wa baba,haguswi eti haramu.

3)ni sisi tulimwamini,kwa tabia ya zamani.
Sasa hatuna imani,imefutika moyoni.
Twahisi baya kichwani,linakuja karibuni.
Huyu mtoto wa baba,haguswi eti haramu.

3)ndege atakapo kufa,huyanyonyoa manyoya.
Kuta linatoa nyufa,jiwe linakuwa boya.
Hongera bwana misifa,jichunge hujacheleya.
Huyu mtoto wa baba,haguswi eti haramu.

5)haki uloiamini,isimamie daima.
Watakuja uwanjani,tutawapiga mtama.
Kifo haisipp nyani,hulia amesimama.
Huyu mtoto wa baba,haguswi eti haramu.

Shairi=MTOTO WA BABA HAGUSWI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom