SHAIRI: Binti Sungura

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,818
2,000
1)Naukumbuka wosia,ule aloniambia
Babu nilipomwendea,ukweli kumwelezea
Umri umeshafikia,wa mke kujipatia
Baba alifurahia,baraka kanipatia
Yupo binti namuoa,katoka kanda ya ziwa.

2)Posa nimeshapeleka,***** ameridhia
Kapokea akicheka,huku katabasamia
Maneno chini kaweka,mwanae kumuusia
Kwangu asijeondoka,laana tamshukia
Posa nimeshapeleka,kwa yule binti sungura.

3)Apendeza akicheka,kwa mwendo anavutia
Mzuri ameumbika,mungu kampendelea
Ukimuona hakika,macho tamkodolea
Avutia akicheka,hapo ndipo nalegea
Mwenzenu nimeshafia,kwa huyo binti Sungura.

4)Sautiye ya upole,siyo kujipayukia
Kama ya nanili yule,jinale nahifadhia
Yule mpiga kelele,mwenye lidomo la bia
Alofukia ndulele,eti akiniwangia
Wangu ushazama,kwa binti Sungura

5)Japo kwao sana mbali,najua tamfikia
Nataka tuwe wawili,ndoa tutajifungia
Ndoa si kama ajali,eti kuiogopea
Haijali yangu hali,yote amekubalia
Macho yangu yamegota,kwa huyu binti Sungura.

6)Wapo watasema sana,hilo sitolihofia
Eti kweli sijaona,mimi tawapuuzia
watachonga na kunena,sisi tutawachekea
Kwingine tena hakuna,hapa nimeshafikia
Maisha nafurahia,kwa huyu binti Sungura

7)Hatari penzi la wizi,hilo sisi twachukia
Leo ninasema wazi,yeye nimemchagua
Hajali ale mandazi,kipo nachompatia
Hakitaji simulizi,mwenyewe anakijua
Matamu yake mapenzi,ya huyu binti Sungura.

8)Tavuka mito na ziwa,ndoa ije kutimia
Nampa jwisi ya miwa,anywa huku asinzia
Gahawa hata halua,vile anaavipendea
Nahisi nilichelewa,mapema ye kumjua
Asali mahaba yake,ya huyu binti Sungura.

9)Mwenzenu nina bahati,Mungu amenishushia
Penzile kama kabati,mwenyewe nalifungua
Wa kwanza fungua nati,hilo ninajivunia
ninampenda kwa dhati,rafikie anajua
Jinale yeye fulani,marufu binti Sungura

SHAIRI-BINTI SUNGURA.
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com

 

Muhsiniina

JF-Expert Member
Oct 31, 2017
326
250
1)Naukumbuka wosia,ule aloniambia
Babu nilipomwendea,ukweli kumwelezea
Umri umeshafikia,wa mke kujipatia
Baba alifurahia,baraka kanipatia
Yupo binti namuoa,katoka kanda ya ziwa.

2)Posa nimeshapeleka,***** ameridhia
Kapokea akicheka,huku katabasamia
Maneno chini kaweka,mwanae kumuusia
Kwangu asijeondoka,laana tamshukia
Posa nimeshapeleka,kwa yule binti sungura.

3)Apendeza akicheka,kwa mwendo anavutia
Mzuri ameumbika,mungu kampendelea
Ukimuona hakika,macho tamkodolea
Avutia akicheka,hapo ndipo nalegea
Mwenzenu nimeshafia,kwa huyo binti Sungura.

4)Sautiye ya upole,siyo kujipayukia
Kama ya nanili yule,jinale nahifadhia
Yule mpiga kelele,mwenye lidomo la bia
Alofukia ndulele,eti akiniwangia
Wangu ushazama,kwa binti Sungura

5)Japo kwao sana mbali,najua tamfikia
Nataka tuwe wawili,ndoa tutajifungia
Ndoa si kama ajali,eti kuiogopea
Haijali yangu hali,yote amekubalia
Macho yangu yamegota,kwa huyu binti Sungura.

6)Wapo watasema sana,hilo sitolihofia
Eti kweli sijaona,mimi tawapuuzia
watachonga na kunena,sisi tutawachekea
Kwingine tena hakuna,hapa nimeshafikia
Maisha nafurahia,kwa huyu binti Sungura

7)Hatari penzi la wizi,hilo sisi twachukia
Leo ninasema wazi,yeye nimemchagua
Hajali ale mandazi,kipo nachompatia
Hakitaji simulizi,mwenyewe anakijua
Matamu yake mapenzi,ya huyu binti Sungura.

8)Tavuka mito na ziwa,ndoa ije kutimia
Nampa jwisi ya miwa,anywa huku asinzia
Gahawa hata halua,vile anaavipendea
Nahisi nilichelewa,mapema ye kumjua
Asali mahaba yake,ya huyu binti Sungura.

9)Mwenzenu nina bahati,Mungu amenishushia
Penzile kama kabati,mwenyewe nalifungua
Wa kwanza fungua nati,hilo ninajivunia
ninampenda kwa dhati,rafikie anajua
Jinale yeye fulani,marufu binti Sungura

SHAIRI-BINTI SUNGURA.
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com

Hahahahaa we IDD wewe! Nilikuwa nafatilia lile shairi ulofuta namba ya "yule" ukamalizia na kapicha, kumbe na huku umemalizia na kapicha pia, dah no more comments
 

Muhsiniina

JF-Expert Member
Oct 31, 2017
326
250
Ila sasa utulie na ww, maana ulipenda usipopendwa ukabutuliwa na kuumizwa, sasa huyu anayekupenda na "kukuheshimu" mthamini, itakusaidia utapiga hatua sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Similar Discussions

Top Bottom