Shairi; Ajali ya basi la Lucky Vicent.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,205
4,403
AJALI YA LUCKY VICENT.

1)Ni msiba wa taifa,umeukumba Arusha.
Tena bila taarifa,kifo hakina bahasha.
Kifo hafanyiwi dhifa,kifo hakina bashasha.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.

2)Ni huzuni kubwa sana,chozi chini ladondoka.
Tumuombe maulana,watoto wameondoka.
Roho zipo kwenye janna,pepo yake msifika.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.

3)Majonzi yametawala,nchi imetikisika.
Tufanye dua na sala,kwa mola rabi rabuka.
Utuepushe inshaala,tusijepata garika.
Poleni wana Arusha,msiba umetupa.

4)Yupo aloita mama,baba yangu ninakufa.
Kwa huzuni kainama,roho ikitoa nyufa.
Kifo hatazami nyuma,huja bila taarifa.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.

5)Kifo hupangwa na Mungu,kukikwepa ni vigumu.
Japo twapata uchungu,hakuna wa kulaumu.
Moyo umepigwa rungu,furaha imekuwa ngumu.
Poleni wana Arusha,msiba umetupata.

6)Nyota zimeshazimika,ni nani wakuziwasha.
Limefika la kufika,gari alipodondosha.
Ziraili malaika,roho ameshasifisha.
Poleni wana Arusha,msiba umetufika.

Shairi=AJALI YA LUCKY VICENT.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom