Ndani ya mkutano Lucky Vicent Arusha kabla ya Polisi kuvamia (+video fupi)

REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,925
14,895
Leo May 18 kwenye shule ya Lucky Vicent Arusha, Polisi walivamia mkutano ulioongozwa na Meya wa jiji hilo akiambatana na viongozi wa dini, Madiwani na Waandishi wa habari ambao Meya alidai lengo lake ni kukabidhi rambirambi walizozichanga wao kutokana na msiba wa ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Wakati viongozi hao wakiendelea kuhojiwa na Polisi Arusha, millardayo.com na AyoTVzinakukutanisha na video ya sehemu ya vilivyokua vinazungumzwa ndani ya mkutano huo kabla ya Polisi kuvamia.

Hii video hapa chini Katibu wa chama cha Wamiliki wa Shule binafsi mkoa wa Arusha Leonard Mao alikua anaongea >>> “Nilitangaza kwa niaba ya Watanzania siku ya kuaga ile miili 35 kwamba tutaendelea kuchanga rambirambi zetu na kwenda kuwaona wale wazazi mmoja baada ya mwingine

“Hakuna hata senti ya mtu itakwenda pembeni…. hatumpi mtu hata kwenye shule ya Vicent, ni waliofiwa wenyewe mkono kwa mkono

FULL VIDEO NDIO HII HAPA CHINI UNAWEZA KUPLAY UKAJIONEZA Zaidi

My take, ni uhuni uliopindukia kuvamia na kuharibu shughuli ya uwasilishwaji wa rambirambi zilitolewa kwa wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki laana iwe juu ya yeyote aliyehusika na uhuni huu.
 
Gambo atakuwa na tatizo la kiutumishi ndio maana kule korogwe alitukana mwanasheria, akazuia ujenzi wa jengo lililokuwa linajengwa karibu na kituo cha mafuta wakati tunaona panone kila kituo kina jengo, Kikwete aliona upuuzi wake atakuja kumuharibia ndio maana aliamua kumtoa kwenye utawala wake kama mkuu wa wilaya, ameshindwa kujirekebisha hata baada ya kukumbwa tena, poleni sana viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom