Arusha: Basi la Asante Rabi lenye namba T 264 linalomilikiwa na tajiri wa shule ya Lucky Vincent, RTO Arusha lifuatilieni miendenendo yake barabarani

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,199
1,346
Wadau habari za asubuhi?, jana nimesafiri kwa gari tajwa hapo juu linalofanya safari zake kutoka mwanza-shinyanga-singida hadi arusha.

Basi hilo kwa kweli limekuwa na tabia ya kutotii sheria za usalama barabarani, yani kuovatake hovyo hovyo bila kufuata sheria kwake ni kawaida. Hadi madereva wa magari mengine huwa wanamunyooshea kidole dereva wa hilo basi kuwa spidi na kuovatake kwake hakufai .

Haya kwa mfano mtu unataka kupanda hilo basi , wahudumu wanakwambia mwisho wa gari hilo ni arusha stand na unaamua kupanda ,mkifika arusha wanakwambia wao hawaingiagi stend badala yake wana stand yao maeneo ya seliani na ndiko wataenda kushusha abiria.

Mfano mtu ulikuwa na safari ya kuunganisha ukifika arusha inakubidi ulipie boda boda uende stand kuu na itakubidi ulipie uzito wa mzigo uliobeba kwa hilo basi na itakubidi ulipie gharama ya kuutoa hapo kwenye stand yao hadi stend kuu.

Abiria tunapazaga sauti zetu askali amfuatilii mnasubiriaga mpake majanga yatokee au mnataka yatokee kama Yale ya tukio la ajali la lucky Vincent ndipo mchukue hatua?.

Muwakanye madereva wa hilo basi waache tabia za kutotii sheria za usalama barabarani na wawashushe abiria wao kwa mujibu wa matamko yao wanapowakaribisha kupanda hayo magari na sio kushusha vichochoroni kwani wanawaongezea gharama zisizo za lazima.

Hizi ndizo taarifa za kiinterijensia RTO arusha tunaomba ulifuatilie gari hilo na muda wowote nitapita maeneo ya ofisi zenu kujua kama mmepata hizi taarifa na kuzifanyia kazi.

Wananchi wanawapa taarifa nyie hamzizingatii badala yake mnasubiria ajali zitokee ndipo mnaanza kuchukua hatua.
 
Mkuu! Wewe una chuki binafsi... Stendi ya seliani ni stendi inayotambulika kushusha abiria hasahasa kwa haya magari ya daraja la juu..kilimanjaro luxury, modern na mabasi mengi ya bei ghali kidogo yanashushia abiria hapo.. Hata kupakia ni hapo hapo
 
Sasa hapa ni Polisi Trafic, au Sumatra? Na kama uwezo wa kufika kituoni unao si unge harakisha ili uya wahi majanga kabla hayaja tokea? Kwanini hukutoa taarifa mapema kabla ya ile ajali ya watoto? Sema una lako jambo.
 
I pad, Chombo la Bosi

Wacha kelele, shukuru mungu umefika salama,
Shukuru mungu kwa kupanda basi zuri kama hili.
FB_IMG_1560573336799.jpg
 
Actualy kile si kidhibit mwendo. Ni AGPS inayomwambia dereva apunguze mwendo pale anapozidi zaid ya 80kms/h. Ila basi bado linauwezo wa kwenda 160km/h

Ok Kumbe? Lakini Madereva wengi wanatembea na 80 kwa sasa,na katika vituo kuna muda wa kufika uliwahi sana utaonekana ulikua unakimbia sana
 
Back
Top Bottom