TANZIA Shaibu Amodu kocha wa timu ya taifa ya Nigeria afariki dunia

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
shaibu.jpg

AMODU


Siku chache baada ya kifo cha Stephen Keshi aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, kocha mwingine wa timu hiyo maarufu kama Super Eagles, Shaibu Amodu naye amefariki dunia, leo.




Amodu amefariki akiwa nchini Benini, siku tatu tu baada ya lifo cha Keshi ambaye pia alifia nchini humo.


KESHI
Wakati Keshi alidaiwa kuwa na maumivu makali ya kichwa, Shaibu amefariki dunia baada ya kulalamika kuwa na maumivu makali ya kifua.

Inaelezwa baada ya kudai kifua kuzidi kuuma, aliamua kwenda kupumzika na hakuamka tena.

Amodu pia amewahi kuifundisha klabu kongwe ya Afrika Kusini ya Orlando Pirates.
 
Dah inasikitisha sana, mzee wa watu amefariki kwa matatizo ya HBP ambayo yamesababishwa na situation yake financially.

Inasemwa kwamba marehemu alikuwa anadai malimbikizo ya fedha zake kutoka NFF na serikalini.

RIP mzee Amodu.
 
Mwezi huu jamani watu wame sepa mfululizo

Huyu jamaa alikuwa na keshi kwenye tim ya taifa miaka ile ya 2000 mwnzoni

R I P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom