Shahidi mkuu kuhusu Rwanda atekwa Kenya

Shahidi mkuu kuhusu Rwanda atekwa Kenya

jMali

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
8,412
Reaction score
5,013
View attachment 203787
Kumbu kumbu ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda

Shahidi mmoja muhimu wa uchunguzi unaofanyika kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda ambaye alikuwa akitarajiwa kuhojiwa na majaji Nchini Ufaransa kuhusu kudunguliwa kwa ndege ya aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, anasemekana kutekwa nyara na kutoweka jijini Nairobi.

Idara ya Polisi Nchini Kenya imekanusha kumtia mbaroni Emile Gafirita.

Majirani wa Emile Gafirita wanasema kuwa walisikia milio ya breki za gari na kamsa pale alipokuwa akirejea nyumbani muda mfupi kabla ya usiku wa manane Jumatatu usiku na kuwaona watu wawili wakimtia pingu na kumrusha kwenye gari.
Idara ya Polisi Nchini Kenya inasema kuwa hawajamtia mbaroni.

Jina la bwana Gafirita liliibuka katika kesi ya hivi majuzi Nchini Rwanda, pale alipotajwa kama askari wa zamani katika kikosi cha ulinzi cha Rais Paul Kagame.

Majaji wawili wa Ufaransa, Marc Trevidic na Nathalie Poux, walikuwa wakipanga kumhoji ili atoe ushahidi mjini Paris kuhusiana na mzinga ulioshambulia na hatimaye kuiangusha ndege iliyombeba Rais wa zamani wa Rwanda hayati Juvenal Habyarimana mnamo mwezi Aprili ya mwaka 1994.

Mauaji ya Habyarimana yaliibua mapigano makali ya kikabila yaliyosababisha mauwaji ya zaidi ya watu laki nane, wengi wao waTusti na wahutu wenye siasa za kadri.


source: BBC

BBC swahili

Chanzo Kingine
View attachment 203788
Shahidi mpya katika kesi ya mashambulizi dhidi ya ndege ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana mwaka 1994 ametoweka tangu Alhamisi Novemba 13 baada ya kutekwa nyara mjini Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na RFI, Emile Gafirita alitekwa nyara mjini humo nje ya nyumba yake mtaa wa Dagoretti muda mfupi kabla ya saa sita usiku baada ya kusimamishwa na watu wawili ambao walimfunga pingu na kumlazimisha kuingia katika gari lao na baadaye kuelekea kusikojulikana.

Polisi nchini Kenya imekanusha kumtia mtu huyo nguvuni ambaye alijulikana kwa majina bandia ya Emmanuel Mugisha na kusema kuwa inachunguza suala hilo ambapo raia huyo wa Rwanda anadaiwa kutekwa na watu ambao kulingana na shahidi wa tukio hilo walikuwa wakizungumza lugha isiyoeleweka, aliiambia RFI.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake raia wa Ufaransa, Wakili François Cantier, Emile Gafirita alikuwa tayari amekabidhiwa mwaliko ili kutoa ushahidi kuhusu tukio la kudunguliwa ndege ya aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana na kumuonya kuhusu usalama wake.

Hadhi ya "Shahidi" ya Emile Gafitira katika kesi hiyo pamoja na majina yake vimekuwa vinajulikana kwa wiki kadhaa zilizopita na pande zote, ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali ya Rwanda ambao baadhi yao wanatuhumiwa katika kesi hiyo.

source: Kesi ya Habyarimana: shahidi mpya raia wa Rwanda atoweka - - RFI

Maoni yangu:
1. Jamaa aliyetekwa alikuwa ASKARI WA ZAMANI WA KIKOSI CHA ULINZI CHA PAUL KAGAME , kama JOEL MUTABAZI ambaye alitekwa nchini Uganda na sasa amefungwa Rwanda. Kama atakuwa hai, basi nategemea ataibuliwa chini ya ulinzi Kigali ambako atashtakiwa kwa mashtaka mbalimbali....Ili mradi tu asiende ku-preempt ushahidi wake dhidi ya kagame kule ufaransa. Is it a coincidence watu wote wanaopanga kutoa ushahidi dhidi ya kagame mahakamani huwa wanauawa au wanatekwa na kwenda kufungiwa Rwanda?

2. Hii move ya kagame inaweza kuharibu uhusiano kati ya Rwanda na kenya kama wakati ule in miaka ya 90 ambapo Kenya ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Rwanda, baada ya kupata ushahidi usiopingika kuwa Rwanda ilifanya ugaidi kama huu Nairobi kwa kumuua seth sendashonga kwa kutumia maafisa ubalozi wake. Seth sendashonga alikuwa anapanga kutoa ushahidi ICTR dhidi ya serikali ya kagame, na vile vile alipanga kutoa ushahidi ufaransa.
Sweden nayo ilishawahi kufukuza ubalozi wa Rwanda mwaka 2012 kutokana na majaribio kama haya ya kufanya ugaidi nchini kwa watu. South africa nayo majuzi ilifukuza mabalozi wa Rwanda.

Hebu tuone kama hii COW itadumu kwa staili hizi maana huyu Uhuru alivyokaa kibiashara anaweza kukubali kuigeuza Kenya iwe kama Uganda (kagame's playground) ambako kagame huwa anafanya anavyotaka.


cc: kadoda11 JustDoItNow R.B sawabho kmbwembwe mjasiria Ngongo majeshi 1981 Gama East African Eagle Kyenju Mgagaa na Upwa ROBERT MICHAEL eliakeem
 
Damu inane a wapendwa damu inanungunika kinachosubiria nimud a mtakuwa mashahidi wa yatakayotokea Rwanda
 
Hii shirika la interahamwe (BBC) naona mwaka huu wameamua...

Ila duuuhhh...hawa watu si watamaliza jameni
 
Hii shirika la interahamwe (BBC) naona mwaka huu wameamua...

Ila duuuhhh...hawa watu si watamaliza jameni
Usianze kujadili shirika(BBC) jadili hoja, PAKA anafanya mbio za sakafuni kama panya ndani ya nyumba, akifika ukingoni atajuta, PAKA anapaswa kujua kuwa hawa anaowanyonga ndugu Zhao ndo wamemzunguka, ndio wanamlinda, ndo wanalinda familia yake na Mali zake zote za wizi, siku ikifika atatamani arudi kwa mseveni
 
Duh mikono ya PAKA inazidi kujaa damu kila siku.
 
Back
Top Bottom