Shaffih Dauda ajirekebishe


Hata mimi nlimsikia akawa anaponda Simba walicheza kwenye eneo lao tu hawakucheza mpira wowote.Nikakumbuka kuwa huyu ni mmoja waandishi wanaosubiri kulipwa chochote ili asidie timu au kiongozi fulani!
 
shafi yuko vizuri kiasi chake, ila jeff leah na oscar oscar wako vizuri saana
 
kumbe hapa issue ni umri sio utendaji kazi, ukweli dogo kapaishwa hajaokoa hata hatari moja ila maneno ya kumpamba yamezidi.
 
Miongoni mwa maajabu niliyopata kuyashuhudia/kuyasikia ni:
1. Mtu kukalia tawi analolikata likiwa juu ya mti.
2. Rafiki yangu mmoja wa Kizungu niliyemonjesha doriani (lile tunda mithili ya fenesi lakini lililo dogo na mviringo zaidi na lenye ncha zilizo kali zaidi linalonukia kama vile limeoza na lenye ladha kama vile limechacha) kwa mara ya kwanza akawa anajilazimisha kulila huku akililaani, na lilipomalizika akanitaka tuagize jengine; tuliishia kuyala matano, na mpaka leo Mzungu huyo ni shabiki namba moja wa tunda hilo.
3. Afisa moja wa jeshi alipokuja likizo kijijini kwetu wakati huo sisi tukiwa wanafunzi wa sekondari alipokuwa akitushajiisha kusoma kwa bidii kwa kusema, 'someni msije mkaishia kuhangaika kama sisi, hii tuifanyayo siyo kazi.' Akaendelea na kazi hiyo hadi alipostaafu kwa kufikia umri, huku akiamini angeruhusiwa kuendelea zaidi.
4. Shehe wa msikitini kwetu ambaye siku zote hutuonya 'msipoteze muda kwa kuwaangalia Manchester United na Van Gaal tu wakicheza na Arsenal au Real Madrid. Hapo Manchester walikuwapo wengi kabla ya hao akina Rooney. Fegerson, Cantona, n.k. Wao wameondoka kwa mafanikio, nyinyi Waislamu wenzangu mnajua mtaondoka vipi kwenda kwa Allah?' Nikashindwa kujua yeye aliwajuaje hao bila ya kufanya hivyo anavyotukataza sisi.
hao wote si tofauti na:
1. Mwandishi anayesema mpira wa Tanzania hauna lolote la kujifunza/kujivunia, wakati 80% ya makala zake ni kuhusu soka la Bongo. 20% iliyobaki ni ya kusifia mpira wa Ulaya kwa kuufananisha na huo anaosema hauna lolote!
2. Mwandishi anayedai kwamba Yanga na Simba hazina lolote jipya, afadhali Azam na Mbeya City, lakini 80% ya makala yake inahusu timu hizo, hizo Azam na Mbeya City anazozisifia hazisifii kuntu (absolutely), hazifananishi zenyewe kwa zenyewe bali ni lazima azihusishe na hizohizo Yanga na Simba, wala hasemi zipi kati ya timu zilizosalia zenye lolote jipya!
3. Wadau wa soka wanaodhani waandishi hao ni mahiri kwa sababu tu makala zao zilisadifiana na utashi wa wadau hao. Siku makala hizo zinapokwenda tofauti nao, waandishi haohao huitwa makanjanja na wadau haohao!
4. Waandishi wanaodai mpira wa Tanzania hauna mvuto, lakini makala zao zimejaa picha za mapambano hayohayo wanayosema hayavutii. Wao wenyewe huwa hawakosi kwenye mechi hizo, na kwenye picha zote za wao kuangalia mechi hizo hatuwaoni kuwa wamefumba macho!
5. Nisaidieni nyinyi wanajmvi!
 

Sasa Kama Hakupata MICHOMO Je Huo Ni UPOPOMA Wa Nani? Jaja Na Coutinyoko AU Owino Na Isihaka? Hivi MAJUZI JAJA BWABWA na COUTINYOKO Hawakucheza? Na Kama Mmeshindwa KURUDISHA Goli 5 Kwa SIMBA Ya Mwaka Jana Na Hii Ya JUZI Basi MSAHAU KUIFUNGA TENA Simba Sports Club ( MNYAMA ).
 
arafu kuna huyu jamaa nae mchambuzi anaitwa oscar naona anakuja kasi sasa wakina shafi inabidi wajiangalie
 

Sasa mbona na wewe umeshindwa kukubali kuwa mtoa mada katoa maoni yake kuhusu uchambuzi wa shafii?

Mtoa mada katoa uchambuzi kwa maoni yake hakuna sehemu ametulazimisha tumuamini anacho sema!

Sijaona wivu,majungu wala usuda ni maoni yake juu ya uchambuzi wa Dauda!
 
Jeff Lea yupo Azam Tv siku hizi kila siku saa mbili usiku. Jeff Lea, ally Mayay na Edo wako juu sana. Hawa wengine umbea na mahaba.

Hata Shaffih yuko vizuri,mi nachomkubali huwa anasema ukweli huwa hana maneno ya kujifariji au kupepesa macho,tatizo letu watz tumewekeza kwenye ushabiki wa Simba,na Yanga kuliko soka kamwe hatutoendelea! Nikirudi upande wa pili ni kuwa yule dogo Manyika alijitahid ila si katika kiwango cha mno,safu ya Yanga ilifanya mashambulizi machache anbayo hayakuwa na madhara ukilinganisha na walichokifanya Simba kwenye safu ya ushambuliaji kipitia kwa Okwi! Ni hayo tu.
 
Tatizo la Dauda ni kutoa mawazo yake kutokana na upepo.
Walimsifia sana Hasheem Thabiti alipofika lakini juzi baada ya kutemwa na timu yake ya Kikapu huko Marekani wakaanza kumponda sana eti safari za kuja Bongo zilizidi na kula sana bata.
Hawa jamaa huwa siwakubali labda yule Alex Lwambano ambaye yeye si mchambuzi bali anasema ukweli tu.
 
Mkuu unajitakia mwenyewe kero kwa kuendelea kuwasikiliza hao jamaa.
Ova
 

that's true,shafii & Luambano Ni wakweli
 

uchambuzi WA soka SI lazima usome,wachambuzi wengi Ni wachezaji WA zamani
 

sema kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…