Shaffi Dauda, umetumia vigezo gani unaposema Samatta atatazamwa/kufuatiliwa na watanzania milioni 4 leo usiku?

Richard,

Watanzania kwa kupinga tu tuko vizuri,wanamichezo wa Tanzania wanapenda kuangalia mechi wakiwa wengi ili wabishane.labda kwenye jiji lako chunguza awa vibanda umiza uwaulize kuhusu mechi ya leo ujue utupe mrejesho
 
Richard,

Kosa la Shafii ni kama la Watanzania wengi tu hata waandishi wa habari kuwa mara nyingine wanatoa / wanaeleza takwimu zisizotokana na utafiti hivyo pia ni MAKANJANJA.

Yaani Wanabuni vitu kutokana na mihemko, hisia au mitazamo yao.

Hapo Shafii amesema hayo mbele ya watu waliozoea na kuzoeshwa kutoa taarifa zenye tafiti.

Mimi ninachojua Watanzania wengi tutamtizama Samatta akicheza uwanjani ila siwezi kusema ni wangapi ila ni Wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Richard,
Watanzania tuko Mil 55 approximately. Tukisema Watanzania Mil 4 wamefuatilia hii mechi tunamaanisha kua kila walipo Watanzania 13 au 14 basi mmoja wao amefuatilia hii mechi kwa Wastani.

Na hao Watanzania 13 au 14 ni mpaka Watoto, Wamama, Wazee,Vipofu, Walioko Vijijini kusiko na Umeme, Wenye hawako na hobby ya mpira, etc.

Kwa muda ule wa Saa tano usiku niseme tu 4mil ni wengi, hatukufikia.
 
Back
Top Bottom