Shaffi Dauda, umetumia vigezo gani unaposema Samatta atatazamwa/kufuatiliwa na watanzania milioni 4 leo usiku?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Mimi ni mpenzi mkubwa wa kituo cha redio cha Talk Sport cha Uingereza ambacho hupasha habari za michezo pekee. Tangu nianze kusikiliza kituo hicho cha redio miaka zaidi ya 15 ilopita nimekuwa ni mfuatiliaji mkubwa sana.

Katika kipindi cha leo mchana ambacho kilikuwa kikiongozwa na watangazaji Paul Hawksbee na Andy Jacobs nilishtuka kusikia wakisema walikuwa wakitaka kufahamu kuhusu Mbwana Samatta na kwamba tayari walifahamu kuwa kuna watanzania ambao wamewasili mjini Birmingham kuangalia mechi.

Mechi ni kati ya timu mpya ya Mbwana Samatta Aston Villa na timu ya Leicester ambayo ni ya marudio ya michuano ya kombe la FA.

Kwanza kabisa nimpongeze Shaffi Dauda kwa kupata fursa adimu ya kusikilizwa na wafuatiliaji wa redio hiyo maarufu nchini Uingereza tena wakati wa mchana ambapo kila mtu yupo mbiombio kurudi nyumbani baada ya kazi.

Dauda ameongea kiingereza kizuri tu na akawa anaeleweka na pia ameonyesha anafahamu anachokiongea kwa kutoa baadhi ya takwimu za kimchezo za Mbwana Samatta.

Pia Shaffi Dauda ameonyesha kwamba hujiandaa kabla ya kuhojiwa khasa na baadhi ya waandishi wa habari za michezo wa kimataifa, hiyo inaweza kumsaidia hata kuweza kuanza kufuatiliwa kwa ukaribu zaidi maana ameonekana na kipaji cha upashaji habari za michezo.

Lakini kuna jambo ambalo nimeona niulize ili kuondoa wingu la mashaka juu ya takwimu sahihi juu ya kwamba wapenzi wa mpira Tanzania ambao watamwangalia Mbwana Samatta leo usiku kwenye hiyo mechi.

Shaffi amedai kwenye kipindi hicho kwamba watanzania wapenzi wa mpira milioni 4 leo usiku wanatarajiwa kufuatilia mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa VIlla Park.

Wao wazungu Paul Hawskbee na Andy Jacobs walionekana kushangaa sana juu ya idadi hiyo na kusema kwa utani kwamba labda Aston Villa imtume Jack Grealish mshambuliaji wa pembeni aende Dar-es-Salaam ili kufahamu ni watu wangapi watajitokeza kumshangaa.

Mara nyingi takwimu kama za idadi ya watu walotazama televisheni hupatikana baada ya kuangalia mitambo na kwamba ni televisheni ngapi ziliwashwa majumbani kuangalia channel inayoosnyesha kabumbu na hapo ndipo mahesabu hufanywa.

Vilevile kutokana na takwimu za nyuma makisio ya idadi ya watu ambao wanatarajiwa kuangalia kituo fulani cha televisheni huwea kutolewa na pia kuweza kuthibitishwa kama kuna ongezeko lolote.

Kwa upande wa Tanzania ni kweli kunaweza kufanywa mfumo huo lakini itachukua muda kuj kupata takwimu sahihi iwe kupitia vituo vya televisheni, redio au simu za mkononi ambazo huunganishwa kwenye mitandao ya internet.

Je, Shaffi Dauda anatumia takwimu zinazotoka kwenye televisheni au simu za mkononi?

Na kama ni hivyo anawezaje kupata idadi hiyo ya watu milioni 4 hata kabla ya mechi haijaanza?

Vinginevyo kwa ushauri tu ni kwamba tunapaswa kuwa makini sana na aina ya habari au taarifa au takwimu tunazotaka kutumia ili kuweza kuwasiliana na vyombo vya habari vya kimataifa kama kituo cha redio cha Talk Sport cha Uingereza.
 
Inahitaji vibanda umiza 40000 vyenye uwezo wa kuingiza watu 80+ nchi nzima.(waliobaki iwe ni wa majumbani) Labda, maana mpaka startimes na azam nafikiri wanaonyesha
 
4m ni ndogo sana labda 7m. Nchi hii ina watu wengi sana wanaofatilia mpira kupitia vibanda umiza na mabar ila sio kwa vinga'muzi vyao binafsi.
 
Back
Top Bottom