Hivi unajua kuwa mpaka sasa Rwanda inapitia Uganda kwenda Mombasa simply kwa sababu kuna kipande upande wa Tanzania hakuna lami? Hivi SGR ikifika kigali Mizigo yote toka Rwanda itapitia Dar ambapo ni karibu na gharama ni nafuu sana. Uamuzi wa kupeleka SGR kwenda Rwanda ni wa kibiashara zaidiSina chochote dhidi ya nchi ya Rwanda. Naangalia data na kufanya mchanganuo. Moja, Rwanda is already in business with Uganda and Kenya. Pili, shehena za Rwanda ni tani laki 9 tu. Hatuwezi kulinganisha na laki 9 za Rwanda na tani milion 3.4 kwenda DRC na Zambia! Ni ukichaa!
Fikiria uamuzi wa kuongeza Terminal III ya Julius Nyerere International Airport. Terminal II ilikuwa imezidiwa kikomo chake cha wasafiri milioni 1.5 kwa kusafirisha zaidi ya watu million 2.4 - ilikuwa inatuumiza sana! Ni uamuzi wa busara kabisa ambao uko supported na data! Terminal III mpya ina uwezo wa kuhudumia wasafiri million 6 - kwa hiyo tutakuwa nayo kwa miaka mingi tu. It is a good investment with a solid business case.
Kwa vile wewe naye si wafanyabiashara! Kawaida ya Mfanyabiashara ni kutafuta fursa mpya baadala ya kuridhika na alizonazo. Ndo maana Dalali ukiwa Mteja wake atakuletea Mchanga ukiwa wa mwisho maana kwake hiyo ni ready money na anahangaika na Mteja mpyaMjadala ni mzuri.
Nipo upande wa mtoa mada.
Kwa nini tusiboreshe TAZARA kufikia kiwango cha SGR? TAZARA inasafirisha tani 187,558 tu wakati ina "potential" ya mamilioni ya tani. Mwaka 2018, Zambia walizalisha copper kiasi cha tani 861,946 (2017 tani 799,329) - halafu tunajua Zambia hawana viwanda vya kuchakata copper. Copper yote inaenda China na nchi nyingine. Je, matani yote haya yalipitia wapi? Je, si kesho kutwa tu Zambia watafikia tani milion moja, moja na nusu, mbili na kuendelea? Je, hatutaki hiyo biashara ya kusafirisha tu? The 2018 copper production hits 861,946 tonnes - Zambia Chamber of Mines
Hapo sijagusa DR Congo!
Kwani huko nchini Rwanda hawakai Binadamu / Watu ambao wanahitaji Huduma? Hivi Watanzania nchi ya Rwanda, Wanyarwanda na Rais wa Rwanda wamewakoseeni nini? Hivi Rwanda ndiyo imewafanya muwe Wavivu, Lege Lege, Goi Goi, Dhaifu Dhaifu na Watu mnaochelewa Kutwa kupiga hatua Madhubuti za Kimaendelo huku mkiwekeza mno katika Majungu, Chuki, Wivu na Uswahili wenu badala ya Kujikita kuangalia kwanini kwa muda mfupi tu huu Rwanda chini ya Rais Paul Kagame inawaacheni Kimaendeleo na hata Wananchi ( Raia ) wake wanazidi kuwa na ' Fikra ' pana kuliko wengi wenu ( japo wapo baadhi wenye Akili kubwa kama za Wanyarwanda ) ila ni wa kuwatafuta sana tena kwa Tochi?
Huwezi linganisha kijiji na Mkoa
Hata TAZARA ni SGR ni vile haitumii umeme
Shida yetu kama taifa miaka yote ni priorities.Kwa vile wewe naye si wafanyabiashara! Kawaida ya Mfanyabiashara ni kutafuta fursa mpya baadala ya kuridhika na alizonazo. Ndo maana Dalali ukiwa Mteja wake atakuletea Mchanga ukiwa wa mwisho maana kwake hiyo ni ready money na anahangaika na Mteja mpya
TAZARA ni SGR sema iwe electrified
Iko hivi reli ikienda rwanda ina maana tutapakia mizigo ya Rwanda halafu kuanzia kigali kwenda Goma na Bukavu ni karibu ina maana drc ya huko itapakia mizigo kwetu, pia bujumbura siyo mbali sana na kigali na usisahau hata kampala nayo siyo mbali na kigali,
So wako sahihi, kuhusu reli kwenda kigoma itaenda baadaye maana kule kuna mji wa uvira ambao mahitaji yao kupata bujumbura ni karibu sana, mji wa kalemie ni mkubwa lkn huwez hata kidogo kuufananisha na Goma na Bukavu! Kwa Congo mji wa kwanza kwa population ni kinshasa ambao hatuwez kuufikia, wa pili ni lubumbashi ambao tunaufikia kwa kupitia Zambia, maana kalemie to lubumbashi ni kama hakuna netwrok ya barabara cause iliyopo ni mbaya kuliko maelezo, so mji wa tatu na wa nne ni Goma na Bukavu ambayo iko karibu sana na Kigali!
Hapo ni Angola na wao wanapambana kukamata mizigo ya Kongo. Hivyo kwa nchi kama kongo ina mibadala mingi sanaView attachment 1236366View attachment 1236367
Shida yetu kama taifa miaka yote ni priorities.
Unakimbilia fursa mpya ilhali uliyonayo tayari hukidhi mahitaji yake! Hiyo siyo biashara ni ubabaishaji tu.
Ndiyo maana mnafunga biashara kila siku.
Hata kwa kutumia common sense tu,Rwamba kuna biashara gani kwa kuliganisha na Zambia?
ACCC CCCçcfccdWanajukwaa,
Nimepitia takwimu kutoka the National Bureau of Statistics (NBS) na Tanzania Ports Authority (TPA) kuhusu mizigo / shehena yanayopitia bandari za Tanzania kwenda au kutoka nchi za jirani.
Kwa mwaka 2017/18, jumla ya tani 5.6 million zilipitia Tanzania (bandari ya Dar es Salaam pekee) kwenda au kutoka nchi za jirani, ikilinganishwa na tani 4.8 million mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la asilimia 17.1 na ni habari njema kabisa kwa TPA na nchi yetu kwa ujumla.
Ukiangalia mchanganuo wa shehena zinazoenda au kutoka nchi za jirani, asilima 61.1% ni za Zambia (36.6%) na J.D. Kongo (24.4%). Hii ni zaidi ya tani 3.4 million ambazo kwa asilimia kubwa zinawafikia jirani zetu kupitia barabara zetu hapa Tanzania. Ukipitia takwimu za 2017/18, TAZARA imefanikiwa kusafirisha mizigo ya tani 187,558 tu (3.4% ya 5.6 million) kwa njia ya reli.
Shehena za Rwanda ni asilimia 16.5% pekee (au tani 922,134) kwa mwaka wa 2017/18. Ukilinganisha na 2016/17, kuna upungufu wa 9.0% - kitu ambacho kinaashiria kuwa mizigo ya Rwanda inawezekana kuwa inapitia Kenya na Uganda.
Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za NBS na TPA wenyewe.
Naomba mwenye taarifa kuhusu ya haya maamuzi ya kupeleka SGR Rwanda atujulishe zaidi.
Nawasilisha.
Huenda kuna secret agreement between our leaders
Mambo ya uchumi wa nchi iwe siri ili kumficha nani?
Mkuu acha uvivu wa kuandika. ChangiaMjadala ni mzuri.
Nipo upande wa mtoa mada.