Elections 2010 SFO yakanusha Taarifa ya PCCB! Suala la Chenge bado halijaisha!

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014


Wakati PCCB wamemshafisha Chenge kwenye kadhia ya Radar kuwa suala hilo limekwisha na Chenge hahusiki, SFO wenyewe wamekanusha kuisha kwa suala hilo na kueleza litatinga mahakama kuu ya Uingereza mwishoni mwa mwezi huu na huko ndiko suala litaamuliwa kama limekwisha au laa.

Taarifa kutoka ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari, umeweka wazi kila kitu kuwa kadhia hiyo bado haijakwisha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kitu ambacho kimekubaliwa kuwa kimekwisha, ni uchunguzi dhidi ya kadhia hiyo ndio umemalizika baada ya BAE kukubali wamegawa rushwa, ila badala ya kuwataja waliowagawia, wamekubali kulipa faini ambayo serikali ya Tanzania, itarudishiwa lile fungu lililokamuliwa ili wakubwa wale.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ubalozini, Mahakama ya Uingereza, inaweza kuamua kuwa hawakubali faini hiyo kulipwa, bali wakalazimisha lazima majina ya walarushwa yatajwe badala na kuzibwa midomo kwa faini na fidia, na kama itakuwa ndio hivyo, tuhuma za Chenge kwenye kadhia hiyo zinabaki kuwa bado ziko pale pale?.

Kama taarifa hii ya ubalozi wa Uingereza ni ya kweli, crdedibility ya PCCB yetu kwenye kuwasafisha mafisadi iko wapi?
 
Kama taarifa hii ya ubalozi wa Uingereza ni ya kweli, crdedibility ya PCCB yetu kwenye kuwasafisha mafisadi iko wapi?.

Ina maana hii taarifa si ya kweli?

Ndugu naomba ufafanuzi tafadhali
 

chenge vidole vya nini?
 
Sasa hawa Mafisadi wa TAKUKUNGURU wamepata wapi kuwa SFO wameona kuwa madai dhidi ya Chenge hayana uthibitisho?....
Pccb yetu wamekalia tu zile nafasi, lakini hawana wajuacho zaidi ya kufuatilia rushwa za buku 5 za uchaguzi!
Shame on them!
 
Ni lini PCCB ilikuwa credible, Richmond ilitosha kuonyesha kwamba they are not credible, not serious and absolutely reckless!
 
Hata kama uingereza wakikubali faini tha fact kwamba wanakubali walitoa rushwa na ndg chenge amekutwa na mabikioni hayo pamoja na dr rashid ambazo ni sehemu ya mkopo kwa tanzania mabao bado tunahangaika watanzania wote kuulipa ; hilo kwetu haliwezi kuisha.
 
Tangu niliposoma ile statement ya PCCB nilishangaa sana kwa sababu najua ile kesi haijapelekwa kwa judge kule UK kwa ajili ya kuamua kuhusu makubaliano ya SFO na BAE Systems. What if akikataa? kwa hiyo PCCB hawakuwa na sababu ya kumsafisha Chenge wakati huu kwani ngoma bado ni mbichi. Huu ni ufisadi kwa upande wa PCCB. Tunasubiri statement yao tena.
 
Chenge hata kama atakuwa cleared bado anatakiwa awaambie Watanzania:

1. $ 1.5 M alizitoa wapi?
2. Consultancy Fees na Personal saving anf Family Heritage anazodai ndo zimempatia hizo pesa ni zipi?
3. Kwa nini alitumia madaraka yake vibaya kuwaweka watanzania katika risk kwa manufaa yake tofauti na matarajio
4. Ameongea nini na PCCB wamemsafisha wakati Mdumange ndo kwanza unaaanza?
 
pccb walifanya uchunguzi wao ******. Hosea nae mtuhumiwa kisha anamlinda mtuhumiwa. Hii yote ni kesi ya nyani na ngedere.
 
''''Taarifa kutoka ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari, umeweka wazi kila kitu kuwa kadhia hiyo bado haijakwisha.''''

Noted with thanks, tusubiri blablaa nyingine

Thisi kantry bwana!
 

Hapo ndipo kwenye goli la kisigino la Chenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…