Agama_Agama
Senior Member
- Sep 13, 2016
- 141
- 135
Nimekuwa nikijiuliza swali hili bila mafanikio ya kupata jibu. Serikali za awamu mbili zilizopita ziligubikwa na kashfa nyingi za ufisadi uliohusisha mabilioni ya shilingi.
Awamu hii ilikuja na kutuaminisha kuwa itapambana na ufisadi na kubana matumizi ya serikali. Haya yalianza kutekelezwa mara tu serikali hii ilipoingia madarakani.
Safari za nje kwa watumishi zikapigwa stop mpaka kipatikane kibali cha mkulu, likaja zoezi la kupunguza matumizi ya vikao, wakasakwa watumishi hewa, ukaja uhakiki wa watumishi (kitu ambacho sijaona tija yake kabisa zaidi ya kuharibu mifumo - creating instability), kuhimiza ukusanywaji wa kodi (tunaambiwa makusanyo yameongezeka) na mengine mengi yaliyolenga kubana matumizi na kuongeza pato la taifa.
Kimtazamo hali hii ilitakiwa kufanya maisha yawe bora zaidi maana mianya ya wapigaji imezibwa. Cha kunishangaza ni kuwa hali imekuwa tofauti katika kipindi cha takriban miaka miwili. Huduma zitolewazo na serikali zimezorota mfano mzuri ukiwa hospitali za serikali. Katika vipindi viwili vilivyopita hakukuwahi kuwa na upungufu wa dawa hospitalini kama tuliouona katika kipindi hiki.
Watumishi wa serikali wamekuwa wakipata nyongeza kwenye mishahara kila mwaka ili kujaribu kufidia ongezeko la gharama za maisha, kitu hicho kimekuwa ni ndoto huku gharama za maisha zikizidi kupanda.
Yapo mengi nayoyafikiria mpaka kujiuliza hili swali, serikali zilizotangulia ziliwezaje kuepuka hii hali ya sasa ikiwa kulikuwa na wapigaji kila sehemu, wafanyakazi hewa, wakwepa kodi na madudu mengine yote?